ZAKAH SEHEMU YA 26
Assalam Alaykum Wa RahamatuLLAH Wa Barakatuh
*KUTOA ZAKAH*
=======🔹🔷🔹
=======
_SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA_
*Swadaqah*
*Aina Za Swadaqah*
```⏯Swadaqah haina maana ya kutoa pesa tu au kumsaidia mtu, bali Swadaqah ziko aina nyingi sana.
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"Kila Muislam anatakiwa atoe Swadaqah".
Wakasema:
"Ee Mtume wa Allaah, asiyekuwa na mali (je)?"
Akasema:
"Afanye kazi kwa mikono yake, ajisaidie nafsi yake kisha atoe Swadaqah".
Wakasema:
"Ikiwa hajapata?"
Akasema:
"Amsaidie mwenye shida".
Wakasema:
"Asipompata?"
Akasema:
"Afanye mema na aache shari, kwani akifanya hivyo anaandikiwa (thawabu ya) Swadaqah".
[Al-Bukhaariy na wengineo]
Na katika riwaya nyingine amesema:
"Kila siku jua linapochomoza nafsi inaandikiwa juu ya kila inachotenda (katika thawabu ya) Swadaqah. Katika hayo ni kuwapatanisha wawili wanaogombana (anaandikiwa mtu thawabu ya kutoa) Swadaqah. Akimsaidia mtu kumnyanyua ili aweze kumpanda mnyama wake, anaandikiwa Swadaqah, akimnyanyulia mzigo wake, Swadaqah, kuondoa udhia barabarani, Swadaqah, neno jema, Swadaqah, na kila hatua anayokwenda msikitini Swadaqah".
[Ahmad na wengineo]
Na akasema:
"Kati yenu kama yupo mwenye kuuogopa moto, basi atoe Swadaqah walau kwa nusu ya tende, na asiyepata, basi kwa neno jema”.
[Ahmad na Muslim]
Na akasema:
"Siku ya Qiyaamah Allaah Atasema:
"Ee mwana Aadam, niliumwa (kwa nini) hukunitembelea?"
Atasema (mwana Aadam):
"Ee Mola, vipi nitakutembelea na wewe ni Mola wa Ulimwengu?"
Atasema:
"Hukujua kuwa mja wangu fulani alikuwa akiumwa na hukumtembelea? Ama ungelimtembelea, ungelinikuta kwake. Ee mwanaadamu nimekuomba chakula na wewe hukunilisha?"
Atasema:
"Ee Mola wangu, vipi nitakulisha na wewe ni Mola wa ulimwengu wote?"
Atasema:
"Hukujuwa kuwa fulani alikuomba chakula na hukumpa. Huelewe kuwa ungelimpa chakula, ungelikikuta kwangu?
Ee mwanaadamu, nilikuomba maji hukunipa".
Atasema:
"Ee Mola wangu, vipi nitakunywesha nawe ni Mola wa Ulimwengu wote?"
Atasema:
"Mtu fulani alikuomba maji, na wewe hukumpa. Ama ungelimpa ungeyakuta hayo kwangu".
[Muslim]
Na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema pia:
"Mtu hapandi kitu au halimi kitu kisha mwana Aadam akala katika mazao hayo au mnyama au chochote ila ataandikiwa kwa ajili yake Swadaqah".
[Ahmad na At-Tirmidhiy]
Na akasema:
"Kila wema ni Swadaqah, na katika wema ni kumkabili mwenzio kwa uso wa bashasha… (uso mkunjufu)."
[Ahmad na At-Tirmidhiy]```
Itaendelea In shaa Allah
*+97433799776*
*RAUDHWATUL ILM*
*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵*
https://t.me/joinchat/AAAAAEiWeE_WKW4ORQxRzw
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments