Header Ads

Header ADS

VISA VYA WALIOKUA WAKITOA SADAKA SEHEMU YA 3

 A'ssalam alaykum Wa Rahamatullah Wa Barakatuh


🛑 *VISA VYA WALIOKUWA WAKITOA SADAKA*


=======🔹🔷🔹

=======


SEHEMU YA 3⃣


*✅Naam tuendelee na kisa chetu katika Qur'an Kama ifuatavyo*


  

Walipoamka asubuhi, wakaitana ili waende shambani kuchuma mazao kama walivyopanga na kuapa. Wakaondoka huku wakinongo'nezana ili mtu yeyote asiwasikie.

 

Wakaenda, lakini walipofika walidhani kuwa wamepotea maana hawakulitambua shamba lao kabisa.  Hapo tena ndio wakatambua kuwa hakika shamba lao ni hilo ambalo limeangamia!  Wakakosa kila kitu, wakaanza kulaumiana wenyewe kwa wenyewe na majuto yakawa  makubwa!

 

 

Kisha tena wakakiri makosa yao na kujirudi nafsi zao wakaomba kwa Rabb wao  Awaghufurie na mwishowe wakawa watu wema.

 

 

Baadhi ya Salaf wamesema kuwa watu hao walikuwa ni watu kutoka Yemen.  Sa'iyd bin Jubayr amesema kuwa: "Ni watu kutoka katika kijiji kilichoitwa Darawaan ambacho kilikuwa ni maili sita kutoka Sanaa."

 

Imesemekena vile vile kuwa ni miongoni mwa Ahlul-Kitaab kutoka Ethiopia. Na Allaah Anajua zaidi [Tafsiyr ya Ibn Kathiyr] 

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Ameelezea kisa hichi katika Suwratul-Qalam kama ifuatavyo:

 

إِنَّا بَلَوْنَاهُمْ كَمَا بَلَوْنَا أَصْحَابَ الْجَنَّةِ إِذْ أَقْسَمُوا لَيَصْرِمُنَّهَا مُصْبِحِينَ﴿١٧﴾

Hakika sisi Tumewajaribu (Maquraysh) kama Tulivyowajaribu watu wa shamba, pale walipoapa kuwa bila shaka watayavuna (mazao yake) watakapopambaukiwa asubuhi.

 

وَلَا يَسْتَثْنُونَ﴿١٨﴾

Na wala hawakusema In-Shaa Allaah.  

 

فَطَافَ عَلَيْهَا طَائِفٌ مِّن رَّبِّكَ وَهُمْ نَائِمُونَ﴿١٩﴾

Basi (shamba lao) likazungukwa na chenye kuzunga (moto) kutoka kwa Rabb wako na hali wao wamelala.

 

 

فَأَصْبَحَتْ كَالصَّرِيمِ﴿٢٠﴾

Likawa kama lilovunwa ikabakishwa majivu meusi.

 

فَتَنَادَوْا مُصْبِحِينَ﴿٢١﴾

Wakaitana, walipopambaukiwa asubuhi.

 

 

أَنِ اغْدُوا عَلَىٰ حَرْثِكُمْ إِن كُنتُمْ صَارِمِينَ﴿٢٢﴾

Kwamba nendeni asubuhi mapema shambani mwenu, mkiwa mnataka kuvuna.

 

 

فَانطَلَقُوا وَهُمْ يَتَخَافَتُونَ﴿٢٣﴾

Wakatoka na huku wanakwenda kimya kimya wakinong’onezana.

 

 

أَن لَّا يَدْخُلَنَّهَا الْيَوْمَ عَلَيْكُم مِّسْكِينٌ﴿٢٤﴾

Kwamba: “Asikuingilieni humo kwa hali yoyote leo masikini.”

 

 

وَغَدَوْا عَلَىٰ حَرْدٍ قَادِرِينَ﴿٢٥﴾

Wakatoka asubuhi mapema kwa kusudio la nguvu, wakidhani wana uwezo (wa kuwazuia maskini).

 

 

فَلَمَّا رَأَوْهَا قَالُوا إِنَّا لَضَالُّونَ﴿٢٦﴾

Basi walipoliona wakasema: “Hakika sisi bila shaka Tumepotea.”

 

 

بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ﴿٢٧﴾

 (Walivyotanabahi!): “Bali sisi tumenyimwa!”

 

 

قَالَ أَوْسَطُهُمْ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ لَوْلَا تُسَبِّحُونَ﴿٢٨﴾

Mbora wao akasema: “Je, sikukuambieni kwanini hamumsabbih (Allaah?)”

 

 

قَالُوا سُبْحَانَ رَبِّنَا إِنَّا كُنَّا ظَالِمِينَ﴿٢٩﴾

Wakasema: “Ametakasika Rabb wetu! Hakika Sisi tulikuwa madhalimu.”

 

 

فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَلَاوَمُونَ﴿٣٠﴾

Wakakabiliana wenyewe kwa wenyewe wakilaumiana.

 

 

قَالُوا يَا وَيْلَنَا إِنَّا كُنَّا طَاغِينَ﴿٣١﴾

Wakasema: “Ole wetu! Hakika sisi tumekuwa warukao mipaka.”

 

 

عَسَىٰ رَبُّنَا أَن يُبْدِلَنَا خَيْرًا مِّنْهَا إِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا رَاغِبُونَ﴿٣٢﴾

 “Asaa Rabb wetu Akatubadilishia lililo bora kuliko hilo hakika sisi kwa Rabb wetu ni wenye raghba.”

 

 

كَذَٰلِكَ الْعَذَابُ ۖ وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَكْبَرُ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ﴿٣٣﴾


Hivyo ndivyo adhabu, na bila shaka adhabu ya Aakhirah ni kubwa zaidi lau wangelikuwa wanajua. [Al-Qalam: 17-33]

 

 Allah anajua zaidi


*☎+97433799776*

*RAUDHWATUL ILM*

*NDOA KATIKA UISLAM*

📗〽〽〽〽〽〽〽〽〽📗


QURAN NA SUNNAH TZ 

WHATSAPP NO +255713849566 


TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾


websites.

http://qurannasunnahtz.blogspot.com/


Facebook page.

https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks


Instagram.

http://www.instagram.com/qurannasunnah


Whatsapp.

https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE


telegram.

https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk


YouTube

http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A



 

No comments

Powered by Blogger.