FUNGA YA ASHURA SEHEMU YA 4
Assalam Alaykum Wa RahamatuLLAH wa Barakatuh
*🌹FUNGA YA ASHURA🌹*
____________________________
*4-Bid'ah Katika Siku Ya 'Aashuraa:*
____________________________
```Katika mwezi huu wa Al-Muharram, siku ya 'Aashuraa (tarehe 10 Al-Muharram) baadhi ya watu hufanya maandamano na kuvaa nguo nyeusi wakidai ni nguo za msiba, na huku wakijipiga vifua kwa ngumi na wengine kujikata kwa visu, kujipiga kwa minyororo na damu kuwamwagika, wakidai wanaomboleza kifo cha Al-Husayn (Radhwiya Allaahu 'anhu). ‘Ulamaa wote wa Kiislamu wamepinga na kukemea mno tendo hilo. Hakika hizo ni tabia na mila za Kimajusi za huko Fursi ambayo ni Iran ya sasa.```
Imaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
*"Bid'ah zinazofanyika katika siku hii ni kuwa baadhi ya watu wameitenga na kuifanya kuwa ni siku ya huzuni kwa kuuliwa Al-Husayn (Radhwiya Allaahu 'anhu). Hivyo watu hulia na kujipiga na hali Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameharamisha hayo kwa dalili:*
عَبْد الله ابْن مَسْعُودٍ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((لَيْسَ مِنَّا مَنْ ضَرَبَ الْخُدُودَ وَشَقَّ الْجُيُوبَ وَدَعَا بِدَعْوَى الْجَاهِلِيَّةِ)) متفق عليه
```Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas’uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Si miongoni mwetu anayejipiga mashavu, akapasua mifuko na akaomba maombi ya kijaahiliyyah)). [Al-Bukhaariy]
Bali juu ya hayo, wanatukana na kuwalaani Maswahaba wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika siku hiyo."
Ibn Rajab amesema:
"Wanayoyafanya Raafidhwah (Mashia) katika siku hii kuwa ni siku ya huzuni kwa ajili ya kuuliwa Al-Husayn (Radhwiya Allaahu 'anhu) ni amali ambazo anazopoteza mtu katika uhai wake akadhani kuwa anafanya amali njema. Wala Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuamrisha kufanya siku za misiba na vifo vya Manabii kuwa ni siku za huzuni, sasa vipi iwe siku ya huzuni kwa wasio Manabii?"
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atuongoze katika njia iliyonyooka na Atuthibitishe nayo. Aamiyn.```
------Mwisho-----
Mwenye swali anaruhusiwa kuuliza.
*+97433799776*
*RAUDHWATUL ILM*
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments