MAKATAZO YA KISHERIA KWA WANAWAKE 4
*🌹🌹Assalam alaykum warahamatullah wabarakatuh*
Makatazo Ya Kishari’ah Kwa Wanawake - 4
*🔷Katazo La Kutoa Chochote Kutoka Katika Nyumba Bila Idhini Yake Mume*
```Katika desturi na kawaida za watu kutoa walichonacho kinapohitajiwa, na wakati mwingine wahitaji hupita katika nyumba na kuomba wasaidiwe na wahusika wa hizo nyumba huwa wako katika shughuli zao za kawaida za kutafuta riziki za halali, hivyo hukutana na wachunga wa hizo nyumba ambao huwafungulia milango na kusikiliza maombi yao; kama haja ya dharura basi huwa hawana budi isipokuwa kuitafutia ufumbuzi kama uko ndani ya nyumba; na kama haja si ya dharura basi si vyema kwa mke kufungua mlango na kujiingiza katika mazungumzo na wasio kuwa Mahaarimu zake; na itapobidi kutoa basi atowe bila ufisadi na atowe kwa ajili ya Allaah na sio kumpatia amtakae kwa sababu duni za kidunia.
Mke ni vyema aelewe kuwa yeyé ni msimamizi na mchungaji katika nyumba ya mumewe na kuwa atakuja kuulizwa kuhusu usimamizi na uchungaji huo.
Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Ee!! Jueni ya kwamba nyie nyote ni wachunga na kila mmoja ataulizwa alichokichunga, kiongozi wa watu ni mchunga na ataulizwa kwa alichokichunga, na mwanamme ni mchunga wa familia wake na ataulizwa kwa alichokichunga, mwanamke ni mchunga wa nyumba ya mume wake na watoto wake naye ataulizwa alichokichunga, na mtumwa ni mchunga wa mali ya bwana wake naye ataulizwa kuhusu uchungaji wake”[Imepokelewa na Al-Bukhaariy, kitabu cha Hajj, milango ya Al-Muhswar na Jaza ya kiwindo, Hadiyth namba 2381 na 2384 na 2560; na katika Kitabu cha Tafsiri Qur-aan, Suuratul Qul A’uwdhu birabbil Falaq, Hadiyth namba 4816 na 4828; na Muslim, katika Kitabu Al-Imaarah, mlango wa fadhila za Al-Imaamu Al-‘Aadil [Muadilifu]……, Hadiyth namba 4314].
Dada yangu katika iymaan fahamu na uelewe kuwa nyumbani kwako kuna majukumu mengi na makubwa mno, kwa hivyo yahifadhi vizuri kwa kuyatekeleza kama ipasavo; ihifadhi mali ya mume wako na katika hiyo mali ni nyumba na kila kilichomo ndani yake.
Hifadhi nzuri ya mali ya mume huwa ni katika mipango mizuri ya kuchunga nyumba kwani huwa iko mbali na ubadhirifu au israfu, pia kutotoa kitu chochote kile hata kiwe kidogo vipi kutoka katika nyumba bila ya idhini ya mume ni katika kuchunga mali ya mume.
Imepokelewa kutoka kwa Abu Umaamah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Asitoe mwanamke kitu chochote kutoka katika nyumba ya mumewe isipokuwa kwa idhini ya mumewe.” [Imepokelewa na Al-Bukhaariy, kitabu cha Nikaah, mlango wa Swawm ya Sunnah ya mwanamke kwa idhini ya mumewe, Hadiyth namba 4823; na Muslim, katika Kitabu cha Zakaah, mlango wa atachotoa mtumishi katika mali ya tajiri wake, Hadiyth namba 1710].
Hadiyth hii inatuongoza na kutubainishai kuwa inampasa mke kupata idhini ya mumewe katika kutoa kitu chochote kile katika mali ya mumewe; na makusudio ya kutoa hapa ni: kutoa mali katika njia za kisharia kama kutoa Zakaah au Swadaqah au kumsaidia mpita njia au aliye haribikiwa na kukatikiwa na msaada.
Mke atakapotoa katika njia hizi za kishari’ah kutoka katika mali ya mumewe kwa shuruti ya kuwepo idhini ya huyo mume [iwe kwa kumtaka idhini au awe amepewa idhini kabla kama ikitokea kuhitajika kutoa basi nimekuruhusu kutoa kiasi kadha na katika jambo kadha] hupata thawabu za kutoa na mume hupata thawabu za uchumaji wa hiyo mali iliyotolewa.
Kutoka kwa mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhiya Allaahu 'anhaa) kwamba Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakapotoa mwanamke kutoka katika chakula cha nyumba yake huyo mwanamke (na katika riwayah: katika nyumba ya mumewe) bila ya kufisidi [uharibifu], atapata ujira wake kwa kile alichotoa, na mumewe atapata ujira wake kwa kile alichochuma...”[Imepokelewa na Al-Bukhaariy, kitabu cha Ijumaa, milango ya ‘amali katika Swalah, Hadiyth namba 1353, 1355 na 1356; na kitabu cha Hajj, milango ya Al-Muhswar na Jaza ya kiwindo, Hadiyth namba 1934; na Muslim, katika Kitabu cha Zakaah, mlango wa ujira wa Mhifadhi [khaazin] mwaminifu na mwanamke ataka
potoa..., Hadiyth namba 1706 na 1707].
Hadiyth imebainisha kuwa wote wawili watapata thawabu [mke kwa kutoa na mume kwa sababu ya mali iliyotolewa ambayo aliichuma]; ni uzuri ulioje kwa mume aliyekarimu kwa mali yake na mke aliyemwepesi kutoa kutoka katika mali ya mumewe bila ya uharibifi na utoaji wenyewe katika Njia ya Allaah.```
*❤NDOA KATIKA USLAM❤*
*☎+97433799776*
*(Tambo)*
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
http://www.instagram.com/qurannasunnah
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
No comments