Header Ads

Header ADS

MAKATAZO YA KISHERIA KWA WANAWAKE 3

 🌹🌹Assalam alaykum warahamatullah wabarakatuh*


Makatazo Ya Kishari’ah Kwa Wanawake - 3


*🔷Katazo La Kujizuilia Kulala [Kustarehe] Na Mume Anapomuhitaji*


```Huu dada yangu katika iymaan ni uwanja wenye hatari kubwa, na wengi miongoni mwa wanawake kwa visingizio visivyokuwa na misingi wameuingia na kugaragara ndani yake; hivyo imewawajibikia kwa hilo laana ya Malaika wa ar-Rahmaan kwa kuwa waume zao hawakuridhika nao bali walighadhibika nao.


Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mume atakapomwita mkewe kwenye kitanda chake [kwa tendo la ndoa] na yule mke akakataa kumuitika, Malaika humlaani mpaka kupambazuke” [Imepokelewa na Al-Bukhaariy, kitabu cha Nikaah, mlango wa atakapolala mwanamke hali ya kuwa amekihama kitanda cha mumewe. Hadiyth namba 4821 na namba 4822; Muslim, kitabu cha Nikaah, mlango uharamu wa mwanamke kujizuilia [kujitenga] na kitanda cha mumewe, Hadiyth namba 2602 na Hadiyth namba 2603 na 2604.]


Hadiyth hii na nyengine kama hii dada yangu katika iymaan inabainisha na kuthibitisha kuwa mume ana haki kwa mkewe kama alivyo na haki mke kwa mumewe; na miongoni mwa hizo haki ni hii haki ya kustarehe na mkewe, na ni haramu kwa mke kujizuilia kutekeleza haki za mumewe ikiwemo hii haki ya kustarehe nae; hivyo wakati wowote ule mke akijizuilia kustarehe na mumewe hujiwajibishia laana ya Malaika [dua ya kumuombea maangamizo ya kufukuzwa kutoka kwenye Rahmah ya Allaah].


Vipi utakuwa ikiwa Malaika wa ar-Rahmaan watakuapiza? Vipi itakuwa hali yako wakati umesimama mbele ya Jabbaar Siku ya Qiyaamah, unahesabiwa amali zako na katika amali zako mbovu na chafu imo hii ya kujizuilia kustarehe na mumeo?


Mke huruhusika kujizuilia kustarehe na mumewe kama atakuwa mgonjwa au ana udhuru wenye kukubalika kishari’ah, kama vile yuko katika siku zake au amefunga Swawm ya waajib, na humuwajibikia kumuitika mumewe kama atamuhitaji wakati wowote ule utakapotoweka udhuru.```


 

Itaendelea In shaa Allah


*NDOA KATIKA UISLAM*

https://t.me/joinchat/AAAAAEyebkF4FS9BJV3hkA

MTARISHAJI

SHEKH TAMBO 

ALLAH AMUHIFADHI WHATSAPP NO+97433799776


WASAMBAZAJI

QURAN NA SUNNAH TZ 

WHATSAPP NO +255713849566 


TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾


websites.

http://qurannasunnahtz.blogspot.com/


Facebook page.

https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks


Instagram.

http://www.instagram.com/qurannasunnah


telegram.

https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk



 

No comments

Powered by Blogger.