MAKATAZO YA KISHERIA KWA WANAWAKE 2
*Makatazo Ya Kishari’ah Kwa Wanawake - 2*
*🔷Katazo La Kudhihirisha Mapambo Kwa Wanaume*
```Allaah Aliyetukuka Anasema: “Na kaeni majumbani kwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijaahiliyyah...…” [Al-Ahzaab 33: 33].
Amesema Mujaahid: “Walikuwa wanawake wanapotoka nje ya nyumba zao hujipitisha mbele za wanaume, na huko ndiko kujishauwa kwa majishauwo ya kijaahiliyyah.”
Amesema Qataadah: “Walikuwa wanawake wanapotoka nje ya nyumba zao, hutembea ovyo pasina hayaa na huku wakijitikisa tikisa, na ndio Allaah Aliyetukuka Akawakataza.”
Amesema Muqaatil bin Hayyaan: “Tabarruj ni pale mwanamke anapokuwa ameweka Khimaar [shungi] kwenye kichwa chake lakini akawa hakuifunga itakiwavo, hivyo mkufu [kidani], vipuli [herini], shingo yake na vyote hivyo vikawa vinaonekana”.
Wanawake wanakatazwa kujishauwa na kujitikisa tikisa wakati wakiwa wako nje ya nyumba zao; na huwa ubaya zaidi pale wanapokuwa wamejipamba kwani kutawapelekea wanaume wawatazame na kuyaona mapambo yao; wanawake hawa huwa na mitindo ya kimaajabu ya kupiga viatu vyao chini na kadhalika.
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Aina mbili za watu ni miongoni mwa watu wa Motoni sijawahi kuziona: Watu ambao wana fimbo [mijeledi] kama mikia ya ng'ombe dume ambazo wanawapigia watu, na wanawake ambao wamevaa lakini wako uchi; wanawashawishi wanaume wawatongoze, na wanaelekea kwao [kwa kuwa warahisi]; vichwa vya wanawake hao kama nundu za ngamia zinazoyumba; hawatoingia Peponi na wala hawatoipata [hawatosikia] harufu yake, na harufu yake inaweza kusikiwa kutoka masafa kadhaa na kadhaa” [Imepokelewa na Muslim, kitabu cha Jannah na sifa za na’iyma zake na watu wake, mlango wa Moto watauingia majabari na Pepo wataiingia madhaifu, Hadiyth namba 5103; na katika Kitabu cha Mavazi na mapambo, mlango wa wanawake Al-Kaasiyaat Al’Ariyaat Al Maailaati.., Hadiyth namba 3978].
Angalia dada yangu katika iymaan makemeo makali hayo na mazito na adhabu inayomsubiri mwenye kujifakharisha kwa uzuri wake na kudhihirisha mapambo yake kwa wanaume wasio kuwa maharimu zake; huenda kwa mwanamke kudhihirisha mapambo yake kwa wanaume hapa duniani ikawa furaha, fakhari, pato zuri [kama wenye kushiriki katika mashindano ya mwanamke mzuri] tija na umaarufu; lakini itakuwa hasara na majuto Siku ya Qiyaamah, kwani itakuwa ni sababu tosha kwa yeye kujiharamishia Jannah na kutumbukizwa Motoni.
Ewe mwenye kuamini Allaah na Siku ya Qiyaamah! Jihadhari na kudhihirisha mapambo yako kwa wanaume wasiokuwa maharimu zako; jihadhari sana na kutojisitiri vizuri kwa hijabu ya kishariy’ah utokapo nje ya nyumba yako, au hata ndani ya nyumba yako wakiwepo wasiokuwa maharimu zako; jihadhari na kujitia manukato, udi na mfano wa hivyo wakati unapotoka nje ya nyumba yako; jihadhari na kupatikana harufu ya manukato yako na wanaume wasiokuwa maharimu zako; yote hayo dada yangu katika iymaan ubaya wake ni wenye kuchukiza kwa Mola wako na ni katika yenye kukupelekea kuwa miongoni mwa wenye kuwajibikiwa adhabu Siku ya Qiyaamah.```
Itaendelea In shaa Allah
*NDOA KATIKA UISLAM*
https://t.me/joinchat/AAAAAEyebkF4FS9BJV3hkA
MTARISHAJI
SHEKH TAMBO
ALLAH AMUHIFADHI WHATSAPP NO+97433799776
WASAMBAZAJI
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
No comments