MAKATAZO YA KISHERIA KWA WANAWAKE 1
*🍃Makatazo Ya Kishari’ah Kwa Wanawake - 1c*
```Na kwa kuwa Uislamu ni Dini ya Muumba wa walimwengu wote, hivyo basi maamrisho au makatazo yake wakati mwingine huja hata kwa waliopewa vitabu kabla ya Qur-aan na wasiopewa vitabu, jambo lenye kubainisha uhakika na ukweli kuwa Dini hii ni Dini yenye kumheshimu na kumthamini kila kiumbe hata awe na kiburi, inadi na ukaidi wa aina yake pekee; kama pale Allaah Anaposema:
“Enyi wana wa Israaili! Kumbukeni Neema Yangu Niliyokuneemesheni, na timizeni Ahadi Yangu, na Mimi nitatimiza ahadi yenu, na Niogopeni Mimi tu. Na aminini Niliyoyateremsha ambayo yanasadikisha mliyonayo, wala msiwe wa kwanza kuyakataa. Wala msiuze Aayah Zangu kwa thamani ndogo. Na Niogopeni Mimi tu. Wala msichanganye kweli na uongo na mkaificha kweli nanyi mnajua. Na simamisheni Swalah, na toeni Zakaah, na rukuuni –inameni- pamoja na wanao rukuu”[Al-Baqarah 2: 40-43].
Pia Allaah Anasema:
“Enyi mlio pewa Kitabu! Aminini tuliyo yateremsha yenye kusadikisha yale mliyo nayo, kabla Hatujazigeuza nyuso Tukazipeleka kisogoni, au Tukawalaani kama Tulivyo walaani watu wa Jumaamosi…” [An-Nisaa 4: 47].
Pia Allaah Anasema:
“Enyi watu wa Kitabu! Msipindukie mipaka katika Dini yenu, wala msimseme Allaah ila kwa lilio kweli. Hakika Masiyhi ‘Iysaa mwana wa Maryam ni Mtume wa Allaah, na neno Lake tu Alilopelekea Maryam, na ni Roho iliyotoka Kwake. Basi Muaminini Allaah na Mitume Yake. Wala msiseme: Utatu. Komeni! Itakuwa kheri kwenu. Hakika Allaah ni Mungu mmoja tu. Ametukuka Yeye na kuwa na mwana.” [An-Nisaa 4: 171].
Katika waraka huu tumejaribu kukusanya MAKATAZO YA KISHARI’AH YENYE KUWAHUSU WAUMINI WA KIKE PEKEEijapokuwa katika hayo kuna yanayowagusa pia Waumini wa kiume; lakini lengo hasa ni kukusanya makatazo yenye kuwahusu dada zetu katika Iymaan; kwani wengi wao huenda wakawa hawaelewi kuwa kuna makatazo na yenye makemeo makali, na pia kwa kuwa wengi katika dada zetu huwa si wenye hima wala hamu ya kutaka kuelewa mafundisho ya Dini yao wachilia mbali kuelewa maamrisho au makatazo ya Mola.
Twamuomba Allaah Aujaalie waraka huu uwe wenye manufaa kwa dada zetu na Awalipe kila la kheri wote walioandika kuhusu mada kama hii jambo lililosaidia na kupelekea kuweza kuyakusanya makatazo haya kwa wepesi; pia twamuomba ar-Rahmaan Awafunue macho, akili na nyoyo kila ataejaaliwa kuusoma na kuwafikishia wengine ujumbe unaotarajiwa au uliokusudiwa na waraka huu.
Allaah na Mjumbe wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wametuhadharisha na kwenda kinyume na Hukumu za Allaah au za Mjumbe Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam); Allaah Amesema:
“Basi na watahadhari wanaokhalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu iumizayo.” [An-Nuur 24: 63].
Pia Allaah Anasema:
“Na anachokupeni Mtume chukueni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho” [Al-Hashr 59: 7].```
Itaendelea In shaa Allah
*NDOA KATIKA UISLAM*
https://t.me/joinchat/AAAAAEyebkF4FS9BJV3hkA
MTARISHAJI
SHEKH TAMBO
ALLAH AMUHIFADHI WHATSAPP NO+97433799776
WASAMBAZAJI
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
No comments