Header Ads

Header ADS

TALAKA 2

 *TALAKA TALAKA*


Ndugu katika imaani tunaendea na darsa letu la talaka


🔹Sehemu ya 2🔹


Hakuna wakati wowote ambapo mume anakubaliwa kisheria kutoa talaka tatu kwa mara moja au kikao kimoja. Kufanya hivyo ni kosa na inahesabiwa kuwa ni talaka moja peke yake katika sheria ya Kiislamu.


Ikiwa mume amemuacha mkewe talaka tatu mara moja huhesabiwa ni moja tu. Ikiwa kwa hilo unamaanisha kumuacha mkeo kwa kumpatia talaka ya kwanza, kisha ya pili mpaka ikafika ya tatu haiwezekani kwa hao wawili kurudiana kama mume na mke mpaka mwanzo mke aolewe na mume mwengine wakutane kimwili kisha aachwe. Hapo utaweza kumrudia tena. Allaah Aliyetukuka Anasema: “Na kama amempa talaka (ya tatu) basi si halali kwake baada ya hayo mpaka aolewe na mume mwengine. Na akiachwa basi hapana ubaya kwao kurejeana wakiona kuwa watashikamana na mipaka ya Allaah. Na hii ni mipaka ya Allaah Anayoibainisha kwa watu wanaojua” (2: 230).


  Haifai kwa watalaka kudhulumiana kwa njia moja au nyingine. Pia haifai kwao kuweka chuki na uadui baina yao na kutoa siri walizoweka baina yao kwa wengine. Kuoana ni kwa wema na kuachana ikiwa hapana budi lazima kuwe kwa wema. Pia haifai kwa mume kuchukua kutoka kwa mtalaka wake alivyompa kamahadiya kwa njia yoyote ile na vile vile si halali kwa mke kuchukua visivyo vyake kwa njia yoyote ile.


 kuhusu neno Talaka Rejea ni kama tulivyolieleza hapo juu kuwa hii ni ile talaka ambayo mume anamiliki haki ya kumrejea mtalaka wake nako ni kumrejea mkewe katika kipindi cha eda la kuachwa talaka ya kwanza au ya pili. Allaah Aliyetukuka Anatueleza: “Na wanawake walioachwa wangoje peke yao mpaka tahara (au hedhi) tatu zipite. Wala haiwajuzii kuficha alichoumba Allaah katika matumbo yao, ikiwa wanamuamini Allaah na Siku ya Mwisho. Na waume wao wana haki ya kuwarejesha katika muda huo, kama wakitaka kufanya suluhu” (2: 228).


pindi mke anapoachwa mume ana wajibu wa kumtizama kwa makaazi, chakula, mavazi, matibabu, na yote anayofanyiwa mke akiwa katika ndoa. Ama katika mali mke hatakuwa na haki yoyote isipokuwa walikuwa na ushirika katika hilo. Ikiwa hali ni hiyo kila mmoja atapata haki yake kama walivyopatana wao katika unyumba wao na ile kazi inavyokwenda. Mke atakuwa na yalemali aliyopatiwa na mtalaka wake wakiwa katika ndoa. Haifai kwa mume kuchukua alivyompa kwa njia yoyote ile. Allaah Aliyetukuka Anatuambia: “Wala si halali kwenu kuchukua chochote mlichowapa wake zenu” (2: 229).


Na pia:


“Na mkitaka kubadilisha mke mahali pa mke, na hali mmoja wao mmempa mali nyingi, basi msichukue katika hayo kitu chochote. Je, mtachukua kwa dhuluma na kosa lilio wazi?” (4: 20).


Na Allaah Anajua zaidi


MTARISHAJI

SHEKH TAMBO WHATSAPP NO+97433799776


WASAMBAZAJI

QURAN NA SUNNAH BLOGGER 

WHATSAPP NO +255713849566 


TEMBLEA BLOGGER YETU KWA KUSOMA DARASA ZETU ZAIDI

 http://qurannasunnahtz.blogspot.com/

No comments

Powered by Blogger.