Header Ads

Header ADS

FAIDA KWA WANANDOA

 *FAIDA KWA WANA NDOA*



*MSIMAMO WA MUME PANAPO TOKEA MATATIZO KATI YA MKEWE NA MAMA YAKE*



✍ *_Sheikh Muhammad bin swaaleh Al-'Uthaymiyn_*



 السؤال :

Swali : 


 فضيلة الشيخ، امرأة تعيش مع زوجها، وأم زوجها في بيت واحد، ولكن أم الزوج تؤذي هذه الزوجة بالكلام، والسب، والشتم، والاحتقار مرات كثيرة، 


Fadhwiilat Sheikh , mwanamke anaishi na mume wake na mama wa mume wake nyumba moja *lakini mama wa mume anamuudhi mke kwa maneno na matusi na Dharau mara nyingi* 



 فهل من حق هذه الزوجة أن تطلب بيتاً لها، ولأطفالها، مع العلم أن أم الزوج يعيش معها زوجها، وابنتها الصغرى، ويستطيعون أن يخدموا أنفسهم بدون تعب؟


Je ni katika haki za mke kuomba nyumba yake ( pekee pasina mama wa mume ) na watoto wake, pamoja na kufaham yakuwa mama wa mume anaishi na mume wake na mtoto wake wa kike mdogo na wanaweza kujihudumia wenyewe bila tabu 



 وما هو الموقف الصحيح للزوج من تصرفات أمه تجاه زوجته؟

 

Na je ni upi msimamo wa mume sahihi katika kuamiliana na mama kutokana na mke huyu ? 



 ثم هل يقال: إن بقاءه مع أمه في بيت واحد مع هذه المشاكل يعد من البر؟ أفيدونا مأجورين.



Kisha inasemwa : Hakika kubakia pamoja na mama katika nyumba moja pamoja na matatizo haya huesabika ni katika wema ? Tupeni faida mtalipwa ( thawabu na Allah ) 



 الجواب :

 *JAWABU:-* 



 إذا كان هذا الشخص يستطيع تعديل هذا الوضع فليعدله، وإذا لم يكن هذا فلا أرى أن تبقى الزوجة مع أم زوجها على هذه الحال ؛


Ikiwa huyu mume anaweza kufanya uadilifu katika hili tukio basi na Afanye uadilifu , *na akiwa hawezi Basi wala sioni kubakia mke pamoja na Mama wa mume katika hali hii*



 لأنه ستكون الحياة نكداً على الزوجة ، وعلى أم الزوج ، وعلى الزوج نفسه ، والقلوب كالزجاج ، إذا انكسر فإنه لا ينجبر .


Kwahakika maisha yatakua Dhiki kwa mke , na kwa mama wa mume na kwa mume mwenyewe , Na nyoyo ni kama Kioo ikivunjika hakika haiungiki ( ni muhali kurudi katika hali ya kawaida kama ilivyokuwa ) 



 فعليك أن تفعل عدة أمور : 


*Ni juu yako kufanya mambo haya:-* 



*أولاً* : انظر من المخطئ.


*Mwanzo :* Tizama ni nani mkosaji 



*ثانياً :* عدّل الخطأ إن استطعت. 


*Pili:* Fanya uadilifu katika kosa hilo ikiwa utaweza 



*ثالثاً :* إذا لم تستطع فليس من المصلحة أن تبقى الزوجة عند أم زوجها مع هذه المشاكل .


*Tatu:* Ikiwa hutaweza si katika kutengeneza kumbakisha mke kwa mama pamoja na matatizo haya 



 المصدر :

Masdar :-


📚 لقاء الباب المفتوح [58] /النكاح والطلاق / عشرة النساء والحقوق الزوجية

[ Liqaau Al-baab Al-mafuuh 58 ]



MTARISHAJI

SHEKH TAMBO WHATSAPP NO+97433799776


WASAMBAZAJI

QURAN NA SUNNAH TZ BLOGSPOT

WHATSAPP NO +255713849566 


TEMBLEA BLOGGER YETU KWA KUSOMA DARASA ZETU ZAIDI

 http://qurannasunnahtz.blogspot.com/

No comments

Powered by Blogger.