ZAKAH SEHEMU YA 12
Assalam Alaykum Wa RahmatuLLLAH Wa Barakatuh
*KUTOA ZAKAH*
=======🔹🔷🔹
======
_SEHEMU YA KUMI NA MBILI_
*Kutoa Panapowajibika*
```▶Inawajibika kuitoa ZAKAAH wakati wake unapowadia, na haijuzu kuichelewesha isipokuwa kwa dharura inayokubalika.
Kutoka kwa Bibi ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema kuwa; Mtume (Swalla Alaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"Haichanganyiki mali pamoja na Zakaah isipokuwa itaiangamiza", na katika riwaya nyingine;
"Inakuwa ishakuwajibikia katika mali yako kuitolea Zakaah, kisha usiitoe, kwa hivyo (mali ya) haramu (isiyotolewa Zakaah) inaiangamiza (mali ya) halali".
[Ash-Shaafi’iy na Al-Bukhaariy katika 'At-Taariykh']```
*Kuitanguliza*
```▶Inajuzu kuitanguliza na kuitoa kabla ya kufikia wakati wake hata kabla ya miaka miwili.
Anasema Ash-Shawkaaniy katika kitabu chake 'Naylul-Awtaar';
"Wanachuoni wengi kama vile Az-Zuhriy na Al-Hassan Al-Baswriy na Maimaam Ash-Shaafi’iy na Ahmad na Abuu Haniyfah wamejuzisha kuitanguliza Zakaah kabla ya kufikia wakati wake".
Ama Imaam Maalik na Sufyaan Ath-Thawriy na baadhi ya Wanachuoni wengine wameona kuwa haijuzu kuitanguliza kabla ya wakati wake, wao wameziegemea zile Hadiyth zinazowajibisha kutoa Zakaah baada ya kukamilika mwaka.
Anasema Ibn Rushd:
"Ikhtilafu iliyopo baina ya Wanachuoni ni kuwa - Zakaah ni ‘Ibaadah au haki iliyowajibishwa kupewa masikini. Wanaosema kuwa Zakaah ni ‘Ibaadah, wao wameifananisha na Swalaah na wakasema kuwa haiwezekani kutolewa kabla ya kufikia wakati wake.
Ama wale wenye kuona kuwa ni haki iliyowajibika, wamejuzisha kuitoa kabla ya kufikia wakati wake ikiwa mtu mwenyewe amejitolea kufanya hivyo".
Ama Imaam Ash-Shaafi’iy ameegema madai yake katika riwaya inayosema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwahi kuchukua katika mali ya Al-‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) na kuitolea Zakaah kabla ya kufikia wakati wake.```
*Kuomba Du’aa*
```▶Inapendeza kumuombea dua mtoaji Zakaah, pale anapoitoa.
Allaah Anasema:
خُذْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ وَتُزَكِّيهِم بِهَا وَصَلِّ عَلَيْهِمْ إِنَّ صَلاَتَكَ سَكَنٌ لَّهُمْ
"Chukua Swadaqah katika mali zao, uwasafishe na kuwatakasa kwa ajili ya hizo (Swadaqah zao) na kuwataja kwa vizuri (mbele yangu) na uwaombee du'aa. Hakika kuwaombea kwako kutawapa utulivu. "
[At-Tawbah: 103]
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Abi ‘Awfiy amesema:
“Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapoletewa mali ya Zakaah akisema: "ALlaahumma salliy ‘alayhim". Na baba yangu siku moja alimpelekea mali ya Zakaah akasema: "Allaahumma salliy ‘alaa aali Abi ‘Awfiy".
[Ahmad na wengineo].
Imepokelewa kutoka kwa Waail bin Hujr kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuombea mtu mmoja aliyeleta ngamia wa Zakaah akasema:
"Allaahumma Baarik fiyhi wa fiy ibilihi". (Allaah mbariki yeye na katika ngamia wake)
Anasema Imaam Ash-Shaafi’iy:
"Ni Sunnah kwa Imaam anapopokea mali ya Zakaah kumuombea dua mtoaji kwa kumwambia: "Aajaraka Allaahu fiyma a’atwayta, wa baarik laka fiyma abqayta".
(Allaah akupe ujira mwema katika ulichotoa na akubarikie katika kilichobaki).```
*Mali Inayotolewa Zakaah*
```1.. Dhahabu na Fedha
2. Mazao na Matunda
3. Mali ya Biashara
4. Wanyama wa kufugwa
Itaendelea In shaa Allah```
*Watts app -+97433799776*
*RAUDHWATUL ILM*
*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LIÑK IFUATAYO⤵*
https://t.me/joinchat/AAAAAEiWeE_WKW4ORQxRzw
SWALI NA JIBU
Sheikh Abuu Muhammad
_حفظه الله ورعاه._
*Tafadhali wasambazie wenzako upate ujira wa kusambaza*. 👆🏽👆🏽
WASAMBAZAJI
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
No comments