ZAKAH SEHEMU YA 13
Assalam Alaykum Wa RahmatuLLLAH Wa Barakatuh
========🔹🔷🔹
========
_SEHEMU YA KUMI NA TATU_
*Dhahabu Na Fedha*
```Allaah Anasema:
وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلاَ يُنفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللّهِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ. يَوْمَ يُحْمَى عَلَيْهَا فِي نَارِ جَهَنَّمَ فَتُكْوَى بِهَا جِبَاهُهُمْ وَجُنوبُهُمْ وَظُهُورُهُمْ هَـذَا مَا كَنَزْتُمْ لأَنفُسِكُمْ فَذُوقُواْ مَا كُنتُمْ تَكْنِزُونَ
"Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa Mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote, japo watakirihika washirikina.
Enyi walioamini! Hakika wengi katika Wanavyuoni mafuqahaa wa dini na Wamonaki wanakula mali za watu kwa batili, na wanazuia njia ya Allaah. Na wale wanaorundika (hazina za) dhahabu na fedha na wala hawazitoi katika njia ya Allaah, basi wabashirie adhabu iumizayo."
[At-Tawbah: 34-35]
Kwa hivyo mwenye kumiliki viwili hivyo (Dhahabu au Fedha) ikiwa ni katika mfumo wa pesa au mikufu au vipande (vinoo), ikitimia Niswaab yake na kukamilisha mwaka na akawa hana deni, wala shida yoyote inayokubalika, anawajibika kuitolea Zakaah yake.```
*Wakati Wa Mtume*
```Wakati wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), watu wa Bara Arabu walikuwa wakifanya biashara zao kwa njia ya kubadilishana bidhaa, na hawakuwa wakitumia pesa isipokuwa wachache sana walioweza kumiliki pesa za dhahabu na za fedha zilizokuwa zikitumika katika nchi za jirani.
Pesa zilizotengenezwa kwa dhahabu zilikuwa zikiitwa Dinari, na zilikuwa zikiletwa kutoka nchi za Warumi kama vile Byzantine na nyenginezo, na walikuwa pia wakitumia pesa zilizotengenezwa kwa fedha zilizokuwa zikiitwa Dirham.
Kwa vile pesa hizo zilikuwa zikiwafikia zikiwa na uzito mbali mbali, na kiasi mbali mbali, nyengine ndogo ndogo na nyengine kubwa kubwa, na hazikuwa na kiasi maalum wala uzito maalum, kwa hivyo watu wa Makka hawakuwa wakizitumia kama zinavyotumiwa pesa za kawaida, bali walikuwa wakizipima na kuzipa thamani maalum waliyokubaliana.
Miongoni mwa vipimo walivyokuwa wakitumia ilikuwa ratili, ambayo wakati huo ilikuwa na uzito wa wakia kumi na mbili na walikuwa pia wakitumia vipimo vya Mithqaal.
Kutokana na kipimo cha Mithqaal, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:
"Haitolewi Zakaah ikiwa dhahabu haikutimia Mithqaal ishirini."
Karatasi za benki (Bank notes) zinazopigwa chapa na serikali tofauti ulimwenguni, hupigwa chapa kulingana na Dhahabu na Fedha inayomiliki serikali hizo, ama sivyo serikali yoyote masikini au yenye madeni ingelipiga chapa idadi ya noti yenye thamani kubwa kuliko dhahabu waliyo nayo na kuweza kulipa madeni yao na kujitajirisha.```
..................
Itaendelea In shaa Allah
*Watts app -+97433799776*
*RAUDHWATUL ILM*
*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LIÑK IFUATAYO⤵*
https://t.me/joinchat/AAAAAEiWeE_WKW4ORQxRzw
WASAMBAZAJI
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
No comments