Header Ads

Header ADS

ZAKAH SEHEMU YA 14

 Assalam Alaykum Wa RahmatuLLLAH Wa Barakatuh


*KUTOA ZAKAH*


=======🔹🔷🔹

=======


_SEHEMU YA KUMI NA NNE_


*Dhahabu na Fedha*

*Niswaab Yake*

 

```Dhahabu hailipiwi kitu mpaka ifikie Niswaab yake na imilikiwe (Niswaab hiyo) kwa muda wa mwaka (Mwaka wa Kiislam).


Niswaab ya dhahabu ni mithqaal 20 au gramu 92 au Tola71/2 au wakia 3. (Baadhi ya Wanachuoniwanasema kuwa Niswaab yake ni gramu 85 au Tola 5 au wakia 2), na hii inatokana na ugumu wa kuweza kukisia bei ya vipimo vilivyokuwa vikitumika wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na vinavyotumika wakati wetu huu. Hapana hitilafu juu ya kiwango cha Mithqaal 20 isipokuwa hitilafu ipo katika kuifasiri Mithqaal katika vipimo vya kisasa.


Inapofikia kiwango hicho, na kubaki muda wa mwaka, unaichukua na kuipeleka kuipima kwa sonara au kwa wajuzi, na baada ya kuijua thamani yake unailipia 2.5% (mbili unusu katika mia) ya thamani ya dhahabu yote.


Niswaab ya dhahabu ndiyo Niswaab ya pesa za kawaida.


Kwa mfano katika nchi ya UAE, bei ya gramu tisini na mbili ya dhahabu ni Dh. 2575/-


Kwa hivyo hicho ndicho kiwango cha kuanzia kulipia Zakaah. Na dhahabu yako inapofikia kiwango hicho unailipia Dh. 64/- ambayo ni mbili unusu katika mia ya thamani hiyo. Dhahabu inapozidi, na Zakaah yake inaongezeka.


Unailipia thamani ya dhahabu tu bila kuhesabu ujira wa mfuo au kazi ya mkono au thamani ya nakshi zake. (Gharama za ufulishaji hazimo).```


*Fedha*

 

```Niswaab ya fedha ni mithqaal 140 au Tola 36 au wakia 141/2.


Ikifikia kiwango hicho na ikamilikiwa muda wa mwaka, inalipiwa moja katika arubaini au mbili unusu katika mia ya thamani yake.

______```


Itaendelea In shaa Allah


*📞+97433799776*

*RAUDHWATUL ILM*


*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LIÑK IFUATAYO⤵*


 https://t.me/joinchat/AAAAAEiWeE_WKW4ORQxRzw


WASAMBAZAJI

QURAN NA SUNNAH TZ 

WHATSAPP NO +255713849566 


TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾


websites.

http://qurannasunnahtz.blogspot.com/


Facebook page.

https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks


Instagram.

http://www.instagram.com/qurannasunnah


Whatsapp.

https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE


telegram.

https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk



 

No comments

Powered by Blogger.