NDOA SEHEMU YA 1
*Assalaam A'laykumu Wa Rahmatullah Wabarakatuh*
🛑 *DARASA LA NDOA* 🛑
[( *عقد الزواج* )]
*SEHEMU YA KWANZA*
===========🔹🔷🔹===========.
*Ndoa* ni Mkataba wa kuwepo kwa maelewano na makubaliano baina ya pande mbili, na kuridhiana baina ya Mke na Mume katika kusimamisha mahusiano ya kisheria baina yao. Na huwakilishwa maridhiano haya katika maneno yanayotamkwa na yenye kupita baina ya hawa wenye kuwekeana mkataba huu, na huitwa kuwa ni *Ijab* na *Qabuul*.
*NGUZO ZA NDOA ( 'AQD*) *NA*
*SHARTI ZAKE*
[{ *أركان العقد وشروطه*}]
==============🔷=============.
Ndoa ( 'Aqd ) inakamilika kwa kukamilika kwa masharti yafuatayo:-
a) *Idhini ya Walii*.
b) *Kuridhika kwa bibi harusi mtarajiwa*.
c) *Kutimia kwa tamko la ndoa yaani Ijaab na Qabuul (yaani iijab na qubuul iliyounganishwa kwa tamko la ndoa au yenye kufidisha maana hiyo)*.
d) *Kuwepo kwa mashahidi wawili waadilifu*.
e) *Kubalighi na kuwa na utambuzi baina ya wanandoa, hivyo haifai kuwepo kwa ndoa ikiwa mmoja wapo ni mwendawazimu au mdogo kwa umri na bado hajabaleghe*.
*TANBIHI*
1⃣ Ndoa ( 'Aqd ) hii inalazimika kwa pande zote mbili husika, ila katika baadhi ya hali kama vile mwanamke kudanganywa na kughuriwa na mwanamme au mwanamme kuoa mwanamke asiyezaa kisha akagundua kuwa hazai na hakujua hilo kabla, *katika hali hii anayo haki ya kuvunja ndoa ( 'Aqd.)*
2⃣ Na kwa hali hiyo hiyo ni kujionesha mwanamme kuwa ni mchaji ALLAAH na mtu mwenye msimamo kisha baada ya muda ukadhihirika ukweli kuwa ni muovu na ni mtu mpotevu hana sifa hizo za mwanzo, *hapa vile vile itavunjika ndoa ( 'Aqd ) yao.*
Na kwa mfano huo huo ni kuoa kwa mwanamme msichana akitegemea kuwa ni *bikra* kisha ikadhihirika kuwa sio *bikra*, au akaona aibu nyingine iliyokuwa ni dhahiri na ya wazi kabisa au maradhi yenye kuchukiza.
⛔ *Dalili ya hayo ni Hadiyth hii* :-
Imepokewa kutoka kwa Ka’ab bin Zaid kuwa Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) alioa mwanamke wa kabila la Banii Ghafaar, alipokwenda kwake na baada ya kuweka nguo zake na kukaa katika kitanda na kuona baina ya kitovu na mbavu weupe ambao ulimuondoa na kukaa mbali nae na kuondoka kitandani, kisha akamwambia:- *“ Chukua nguo zako.” na hakuchukua alichompa (katika mahari.)*”
*( Ahmad )*
Amesema 'Umar bin al-Khattwaab (Radhiya ALLAAHU 'anhu) kwa yule bwana aliyeoa mwanamke nae (mwanamme) hazai, *‘Mwambie kuwa wewe huzai na mpe uhuru wa kuchagua.’*
Itaendelea In Shaa ALLAAH
*☎+97433799776*
*NDOA KATIKA UISLAM*
*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵*
https://t.me/joinchat/AAAAAEyebkF4FS9BJV3hkA
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments