SUBIRA NJEMA
*🌹EWE ULIEKATA TAMAA NA REHMA ZA ALLAH...SOMA HII UTAPATA KITU*
*Subira Njema صَبْرٌ جَمِيلٌ*
🎈🎈
*Subira Za Maswahaba - Tamaadhwur Bint Al-Sulaymiyyah – Al-Khansaa (رضي الله عنها)*
```Jina lake hasa ni Tamaadhwur bint 'Amru bin Ash-Shariyd bin Rabaah As-Sulaymiyyah. Alijulikana kwa jina la Al-Khansaa na vile vile Umm Ash-Shuhadaa (mama wa mashahidi) kutokana na watoto wake waliofariki katika Jihaad. Pia alijulikana kuwa ni mwanamke mwenye haiba nzuri iliyojaa fadhila, tabia njema, ushujaa na subira kubwa.
Kabla ya kuingia katika Uislam, alikuwa akitunga mashairi ya beti mbili tatu hadi walipofariki kaka zake Mu'aawiyah na Swakhar bin 'Amru, alifikwa na huzuni kubwa sana hata akawatungia mashairi. Yakawa mashuhuri mno, hata yakazidi kumpatia umaarufu. Na imesemekana kwamba hakuweko mwanamke aliyekuwa hodari wa mashairi kama yeye.
Baada ya vifo vya kaka zake, alikuja kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) pamoja na watu wake wa Banu Sulaym akasilimu. Ilipofika wakati wa vita vya Qaadisiyyah alidhihirisha subira yake kubwa alipokwenda vitani pamoja na watoto wake wanne wa kiume na akawausia kwa kuwaambia maneno haya mazito:
"Enyi watoto wangu, naapa kwa Yule Ambaye hakuna Apasaye kuabudiwa ila Yeye, nyinyi ni watoto wa baba mmoja, sikumkhini baba yenu, mmesilimu kwa kutii, mmehama kwa khiari yenu…" Akaendelea kuwanasihi hadi akasema "Mtakapoamka kesho In shaa Allaah kwa salama, nendeni vitani kupigana na adui zenu, kwani mnajua Aliyowaandalia Allaah (سبحانه وتعالى) ya thawabu nyingi kwa kupigana na makafiri. Tambueni kuwa nyumba ya milele (Pepo) ni bora kuliko nyumba ya kutoweka (Dunia), Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اصْبِرُواْ وَصَابِرُواْ وَرَابِطُواْ وَاتَّقُواْ اللّهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ))
((Enyi mlioamini! Subirini, na shindaneni kusubiri, na kuweni macho, na mcheni Allaah, ili mpate kufanikiwa))[ Aal-‘Imraan 3: 200]
Wakaenda vitani na alipopata habari ya vifo vyao wote alisema: "AlhamduliLlaah kwa Yule Aliyenipa heshima ya kuuliwa kwao na namuomba Allaah (سبحانه وتعالى) Aniunganishe nao kwa Rahma Zake."
Al-Khansaa (رضي الله عنها) akaendelea kubakia katika subira na kuthibitika katika imani yake hadi alipoaga dunia wakati wa ukhalifa wa 'Uthmaan bin 'Affaan (رضي الله عنه) .
Al-Khansaa (رضي الله عنها) ametuonyesha mfano bora kabisa wa Subira Njema kwa kuridhika na majaaliwa ya Allaah (سبحانه وتعالى) na inapasa mzazi anayefiwa na mwanawe afuate nyayo zake.```
WASAMBAZAJI
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments