NDOA SEHEMU YA 6
*Assalaam A'laykumu Wa Rahmatul LLAAHI Wa Barakaatuh*
🛑 *KUTANGAZA NDOA* 🛑
[( *إعلان الزواج* )]
```SEHEMU YA SITA```
==============🔹🔷🔹===========
Inapendeza kutangaza ndoa kishari'ah kwa kauli yake Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) :-
" *أعلنوا هذا النّكاح , واجعلوه في المساجد*"
🔺 *Maana yake*
“ Tangazeni ndoa hii, na ifanyeni Msikitini.”
( *At-Tirmidhiy na Ahmad*)
⏯ Na Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) akasema tena:-
" *فصل ما بين الحلال والحرام الدّفّ والصّوت*"
🔺 *Maana yake*
“ Mpaka wa baina ya halali na haramu ni dufu na sauti .”
( *At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah*)
⛔ *TANBIHI*
Na inawezekana kutangaza ndoa Msikitini kwa sharti ya kuwa mas-alah ya kuimba na dufu yawe nje ya Msikiti ili kuchunga adabu za Msikiti. Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) alikuwa akichukia sana ndoa kufanywa siri hadi ipigwe dufu na isemwe :- *“Tumewajia tumewajia, tusalimieni nasi tuwasalimie*.” (Ahmad)
⏯ Na si vibaya kusheherekea ndoa kwa kuimba kwa lengo la kuzichangamsha nafsi, kwa sharti kuwa nyimbo hizo ziwe zimeepukana na matusi na uchafu wa maana mbaya na pia ni lazima ziwe nzuri zisiwe zenye kuhamasisha matamanio na kuwatoa watu haya.
Bibi 'Aaishah (Radhiya ALLAAHU 'anha) alisherehekea harusi ya al-Farigha bint Asad na akamsindikiza hadi kwenye nyumba ya mume wake, Nabiit bin Jaabir al-Answariy. Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) akauliza kumuuliza bibi 'Aaishah:-
*يا عائشة , ما كان معكم لهو؟ فإنّ الأنصار يعجبهم اللّهو*
🔺 *Maana yake*
“Ee 'Aaishah, je, hamkuwa na Lahwu (kucheza na kujipumbaza) ?! Kwani Answaar huvutiwa na Lahwu.” ( *Al-Bukhaariy*)
⏯ Hali kadhalika imepokewa na bibi 'Aaishah (Radhiya ALLAAHU 'anha) kuwa Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) amesema: *“Hukumfanyia fulani-kwa mayatima waliokuwepo kwake.”* nikajibu: *tumempeleka kwa mumewe*, akasema: “ *Je, mlikwenda pamoja na kijakazi akapiga dufu na kuimba*”, bibi Aisha akasema aseme nini? Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) akasema: *“Aseme:*
*أتيناكم أتيناكم* *فحّيونا نحيّيكم*
*ولولا الذّهب الأحمر* *ما حلّت بواديكم*
*ولولا الحنطة السّمرا* *ما سمنت عذاريكم*
🔺 *Maana yake*
" *Tumewajia tumewajia,* "
" *Tusalimieni tuwasalimie* "
" *Na kama si dhahabu nyekundu* "
" *Msingeacha vijiji vyenu* "
" *Na kama si ngano nyeusi*"
*"Basi wasingenenepa binti zenu*"
⏯ Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik amesema: *“Alipita Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) mwanzoni mwa kuhamia kwake Madiynah akiwa na harusi pamoja na wanawake, na mmoja wao alikuwa akisema:
*Na akazawadiwa Kondoo akipiga ukelele mkubwa kabisa*
*Na mumeo yupo Shamba na unajua ya kesho*.
Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) akasema: *“Usiseme hivyo bali sema:*-
*أتيناكم أتيناكم* *فحّيونا نحيّيكم*
" *Tumewajia tumewajia,* " " *Tusalimieni tuwasalimie* "
Itaendelea tena In Shaa ALLAAH
*☎+97433799776*
*NDOA KATIKA UISLAM*
*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵*
https://t.me/joinchat/AAAAAEyebkF4FS9BJV3hkA
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments