Header Ads

Header ADS

NDOA SEHEMU YA 5

 

*Assalaam A'laykumu Wa Rahmatul LLAAHI Wa Barakaatuh*

Tunaendelea na Darasa letu la Ndoa baada ya kuona WASIA Wa *Baba* kwa *Bint Yake* na Kwa *Mkwe Wake* , Leo tena  tupo katika kipengele hiki cha WASIA na tunaona Wasia wa *Mama*  Kwa *bintiye*

🛑                 *USIA WA MAMA*             🛑
                         *KWA  BINTIYE*
                        [( *وصيّة الأم لا بنت* )]
                    ```SEHEMU YA TANO```
============🔹❤🔹=============.
Na hii ya Wasia Wa Mama kwa binti yake  vile vile  ni Sunnah iliyothibiti kwa akina Mama kumuusia bint yao  kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:-

🔺 *Dalili*
Amru bin Hujri aliposa kwa Malik kan-da, kumposa Ummu Iyaas binti Auf bin Muhalim Asshaybaniy, na ilipofika siku ya sherehe ya ndoa yake Mama yake Umama bint al-Harith alichepuka nae pembeni na kumuusia, Kama ifuatavyo :-

⏯ ‘Ee, Binti yangu:- *Hakika usia ukiachwa kwa fadhila ya adabu (yaani isingekuwa na haja ya kuwausia wenye adabu nzuri) ningeliacha kwako, lakini usia mwanangu ni ukumbusho kwa msahaulifu, na msaada kwa mwenye akili. Na lau kwamba mwanamke asingemuhitajia mume basi wazazi kadhalika wasingehitajika. Ni muhimu sana haja zao kuwa pamoja, basi mimi ningekuwa ni mtu nisiyemhitajia baba yako, lakini mwanangu wanawake kwa wanaume wameumbiwa, na wao wameumbwa kwa ajili ya wanaume*.

⏯ Ee, Binti yangu:- *Hakika wewe unaacha mazingira uliyoyazoea na unaacha maisha uliyokulia, unakwenda usipopajua na mwenza usiyemzoea, na atakuwa ndie mwangalizi wako, hivyo basi kuwa kwake kijakazi nae atakuwa ni mtumwa wako asiyetamani kukukosa*.
Hifadhi kwake mambo kumi, atakuwa kwako hazina:-

1 ) *Unyenyekee kwake kwa kukinai*.

2 ) *Umsikilize vizuri na kumtii*.

3 ) *Na uangalie maeneo ya macho yake na pua yake.*

4 ) *Hivyo basi, macho yake yasione au kuangalia yanayochukiza kwako na wala yasinuse ila harufu nzuri kutoka kwako.*

5 ) *Angalia wakati wake wa kulala na chakula chake.*

6 ) *Kwani hakika mbabaiko wa njaa unaunguza na kukosa usingizi kunaghadhibisha.*

7 ) *Chunga mali yake na ulinde heshima yake na watoto wake*.

8 ) *Na matumizi ya mali yawe mazuri na katika kuishi nae upange vizuri maisha.*

9 ) *Usimuasi kwa jambo na usitoe siri zake.*

10 ) *Kwani wewe ukikengeuka na amri yake utapandisha chuki na hasira katika kifua chake, na ukitoa siri zake hutosalimika kwa kumvunjia ahadi yake, kisha ole wako na kufurahi hali yakuwa hana raha, na kukasirika hali ya kuwa amefurahi*.

                      *WASIA WA  MUME*
                            *KWA MKEWE*
                 [( *وصية الزّ وج إلى زوجته* )]
============== ❤ ==============.
Na'am na Imethibiti pia kwa mume kumpa Mkewe Wasia kwa kuona katika Hadiyth hii ifuatayo:-

🔺 *Dalili*
Amesema Abu Dardaai kumuusia mkewe:-

1 ) *‘" Ukiniona mimi nimekasirika jaribu kuniridhisha, nami nikikuona umekasirika nitakuridhisha, vinginevyo hatutoweza kukaa pamoja.*’"

⏯ Na  vile vile akasema mmoja wa waume kumwambia mke wake:-

2 ) " *Chukua msamaha wangu yatadumu mapenzi yangu (mawadda)*, "

3 ) *Wala usizungumze katika kilele cha ghadhabu pindi ninapo ghadhibika.*

4 ) *Wala usinigonge kwa mgongo wako hata mara moja Kwani wewe hujui ni wapi jua linapozamia*

5  " *Na wala usizidishe malalamiko na nguvu kuondoka , Na moyo wangu ukakukataa, na mioyo hugeuka* "

6 ) *Nami nimeona mapenzi katika moyo na maudhi vile vile Zikikutana, basi mapenzi hayakai yataondoka.*


In Shaa ALLAAH itaendelea

*☎+97433799776*
*NDOA KATIKA UISLAM*

https://t.me/joinchat/AAAAAEyebkF4FS9BJV3hkA

QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566

TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾

websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/

Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks

Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah

Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE

telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk

YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A

 

No comments

Powered by Blogger.