Header Ads

Header ADS

NDOA SEHEMU YA 4

 *Assalaam A'laykumu Wa Rahmatul LLAAHI Wa Barakaatuh*


Na'am tunaendelea na Darasa letu la Ndoa na Alfajiri hii tutazungumzia katika kipengele cha WASIA 


🛑 *KUMUUSIA MKE* 🛑

                      [( *استحباب وصية الزوجة* )]

                ```SEHEMU YA NNE```

============🔹🔷🔹============.

Kuwahusia Wanandoa ni katika Sunnah na ni mwenendo mzuri kwani ndani ya ndoa kuna mambo mengi sana na hii ni kutokana na malezi ya kila mmoja alivyolelewa kwao, Kwahiyo kila mmoja anaondokana na yale Malezi ya Maisha aliyoyazoea na kuanzisha Upamoja wao na family yao , hivyo basi hapa panahitaji Subra na Moyo wa kuvumiliana na hii ni kutokana na Wengi wetu kutofahamu haki ya kila mmoja kwasababu ya kuyakimbia Mafunzo Sahihi ya dini yetu. Na Ushahidi wa Usia ni kama tutakavyoona katika Hadiyth hii :-


🔺 *Dalili*

  Anas amesema:- " *Walikuwa Masahaba wa Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) anapoelekea Mke kwa Mumewe, wanamuhimiza katika kumuhudumia mumewe na kuangalia na kuchunga haki zake.* "

 


           

                   *WASIA WA BABA*

                   *KWA BINTI YAKE*

                          [( *وصيّة الأب ابنته* )]

==============🔷=============.

Na vile vile baba ana nafasi ya kumuusia bint yake kama tunavyoona katika hii ya Swahaba Wa Mtume wetu Muhammad ( صلى الله عليه وآله وسلم ) Alivyokuwa akimuhusia Mwanae 


🔺 *Dalili*

'Abdullaah bin Ja'far bin Abi Twaalib amemuusia binti yake kwa kumuambia, *" Ole wako na wivu, nao ni ufunguo wa Talaka*. *Na ole wako na malalamiko mengi, nayo hupelekea katika bughudha*. *Na jitie wanja kwani huko ndiko kujipamba kuzuri zaidi*. *Na kizuri katika vizuri zaidi ni Maji.’* "


                *WASIA WA BABA* 

               *KWA MKWE WAKE* 

                            [( *وصيّة العم لصهره* )]

=============🔷==============.

Na vile vile pia ni katika Sunnah kwa baba kumuusia Mkwe Wake Ushahidi Wa hili ni Hadiyth zifuatazo:- 


🔺 *Dalili*

'Aliy bin Abi Tawalib (Radhiya ALLAAHU 'anhu) alipo posa kwa Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) kumposa mtoto wake Fatma, alisema Mtume juu yake sala na salamu:-

 

" *هي لك على أن تحسن صحبته*"

 

“ *Huyo ni wako maadamu utaufanyia uzuri usuhuba wake.”* [( Imepokewa na Abu Na'iym )]. 

 

Na Hadiyth nyingine ni hii :-


🔺 *Dalili*

Na 'Uthmaan bin Anbasa bin Abi Sufyaan akaposa kwa 'Ami yake 'Utbah kutaka kumuoa binti yake, akamkalisha ubavuni mwake na akaanza kupangusa kichwa chake, kisha akamwambia, *‘ Mtu wa karibu zaidi (ndugu) amemposa ninayempenda zaidi, siwezi kumrudisha, na sina sababu ya hilo. Nimekuozesha nawe ni azizi kwangu zaidi kuliko binti yangu, naye moyo wake umegandana nami zaidi kuliko wako, hivyo mkirimu na ulimi wangu utaona tamu kukutaja, wala usimshushie hadhi yake ikapungua hadhi yako kwangu, na nimekuweka karibu pamoja na ukaribu wa udugu tulionao, hivyo basi usiupeleke moyo wangu mbali na moyo wako.’*


In Shaa ALLAAH itaendelea tena kwa kuona Usia kutoka kwa Mama


*☎+97433799776*

*NDOA KATIKA UISLAM*


*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵*


https://t.me/joinchat/AAAAAEyebkF4FS9BJV3hkA


QURAN NA SUNNAH TZ 

WHATSAPP NO +255713849566 


TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾


websites.

http://qurannasunnahtz.blogspot.com/


Facebook page.

https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks


Instagram.

http://www.instagram.com/qurannasunnah


Whatsapp.

https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE


telegram.

https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk


YouTube

http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A



 

No comments

Powered by Blogger.