NDOA SEHEMU YA 3
*Assalaam A'laykumu Wa Rahmatul LLAAHI Wa Barakaatuh*
🛑 *KUTANGULIZA* 🛑
*NA*
*KUCHELEWESHA MAHARI*
*المعجّل والمؤجّل*
```SEHEMU YA TATU```
=============🔹🔷🔹===========.
Inafaa na inajuzu kutanguliza na kuchelewesha mahari. Kulipa mwanzo na nyingine kuchelewa kama ilivyo kuwa ni ada na desturi ya mahala na uwezo wa mtu.
Lakini kinachofaa zaidi ni kutanguliza chochote kwa yaliyopokewa na ibn Abbas kuwa Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) alimkataza Ali kumuingilia bibi Fatma mtoto wake hadi awe ametoa chochote katika mahari. Ali (Radhiya ALLAAHU 'anhu) akasema kumwambia Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) , ‘Sina chochote’. Akasema Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) : ‘Liko wapi deraya lako la kihutwamiyya?’ Akampa ikawa ndio mahari yake.” (Abu Daawuwd, An-Nasaaiy na Ahmad)
Na akasema bibi 'Aaishah (Radhiya ALLAAHU 'anhaa) : “Ameniamrisha mimi Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) nimuingize mwanamke kwa mumewe kabla hajampa chochote.” (Abu Daawuwd).
*WAJIBU WA MUOAJI*
=========================
*Ni Wajibu* Wa Mwanamme kutayarisha anachokihitaji bibi harusi katika vyombo vya nyumbani kama vile fanicha ili aweke nyumbani kwake. Kilichozoeleka ni kuwa Bibi harusi na ndugu za bibi harusi ndio wenye kutayarisha vyombo hivyo na kuvipanga na kuitengeza nyumba, na wengineo huwa wana tabia ya kuvionyesha vyombo hivyo kwa sherehe na hafla za wazi. Leo hii sherehe kama hizi zinaishia katika mitaa wanayoishi watu wa hali ya chini, ‘Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) alimtayarishia vyombo bibi Faatwimah ndani yake pana nguo zilizofumwa kwa manyoya ya mbuni, na kiriba cha kuwekea maji na mto wa kulalia uliowekewa mmea wenye harufu nzuri.’ (An-Nasaaiy).
Mwanamme huwa ndie muhusika haswa wa kukamilisha kinachohitajika katika nyumba kama vile vyombo na vitu vingine vya ndani ya nyumba. Kishari'ah hakuna uhusiano wa vitu hivyo na mwanamke, ila alichokipenda kukifanya yeye mwenyewe kwa mapenzi yake.
📚 In Shaa ALLAAH itaendelea
*☎+97433799776*
*NDOA KATIKA UISLAM*
*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵*
https://t.me/joinchat/AAAAAEyebkF4FS9BJV3hkA
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments