ZAKAH SEHEMU YA 30
Assalam Alaykum Wa RahamatuLLAH Wa Barakatuh
*KUTOA ZAKAH*
=======🔹🔷🔹
=======
_SEHEMU YA THALATHINI_
*Wanaostahiki Zakaah*
```Swadaqah ya kawaida, anapewa mtu yeyote hata akiwa si Muislam, ama Zakaatul Fitwr wanapewa watu wa aina mbili tu, nao ni masikini na mafakiri Waislam.
Zakaatul Maal (Zakaah ya mali), hii wanapewa aina 8 tu ya Waislamu waliowataja na Allaah katika kitabu chake kitukufu Aliposema:
إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاء وَالْمَسَاكِينِ وَالْعَامِلِينَ عَلَيْهَا وَالْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ وَفِي الرِّقَابِ وَالْغَارِمِينَ وَفِي سَبِيلِ اللّهِ وَابْنِ السَّبِيلِ فَرِيضَةً مِّنَ اللّهِ وَاللّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ
"Swadaqah hupewa (watu hawa):-
1. Mafakiri na
2. Masikini na
3. Wanaozitumikia na
4. Wanaotiwa nguvu nyoyo zao (juu ya Uislam) na
5. Katika kuwapa uungwana watumwa na
6. Katika kuwasaidia Wenye deni na
7. Katika (kutengeneza) Mambo aliyoamrisha Allaah na
8. Katika (kupewa) Wasafiri (walioharibikiwa).
Ni faradhi inayotoka kwa Allaah, na Allaah ni Mjuzi (na) Mwenye hikima".
At-Tawbah: 60.
Ayakayeichunguza aya hii ataona kuwa Allaah ametumia neno 'Lil' katika kuwataja watu aina nne wa mwanzo wanaostahiki kupewa Zakaah. Na hii inaitwa Laam ya tamliyk, na maana yake ni kuwa lazima kuwamilikisha watu wa aina nne wa mwanzo (yaani kuwapa mikononi mwao) Zakaah yao.
Allaah Anasema:
إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاء وَالْمَسَاكِينِ وَالْعَامِلِينَ عَلَيْهَا وَالْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ
Ama katika aina nne waliobaki, Allaah ametumia neno 'Fiy'. Na kwa kutumia neno hilo Allaah hatulazimishi, kuwamilikisha kwa kuwapa Zakaah yao mikononi mwao.
Allaah Anasema:
وَفِي الرِّقَابِ وَالْغَارِمِينَ وَفِي سَبِيلِ اللّهِ وَابْنِ السَّبِيلِ
Kwa hivyo katika aina nne za mwisho, kwa mfano kama unataka kumsaidia mwenye deni, hulazimiki kumpa pesa hizo mkononi mwake, bali unaweza kwenda kumlipia deni hilo moja kwa moja bila ya kumkabidhi mdaiwa huyo pesa hizo mkononi mwake. Hata hivyo, ukitaka unaweza pia kumkabidhi mweyewe mkononi mwake.
Ukitaka kuzitumia pesa za Zakaah katika njia ya Allaah, unaweza kununua kwa mfano silaha na kuwakabidhi wapiganaji 'Mujaahidiyn' au unaweza kuzitumia katika njia ya Allaah bila ya kumkabidhi mtu pesa hizo mkononi mwake, wakati huo huo unaweza ukitaka kuwakabidhi wanaohusika au wajuzi ili ipate kutumika kwa usahihi zaidi.```
Itaendelea In shaa Allah
*+97433799776*
*RAUDHWATUL ILM*
*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵*
https://t.me/joinchat/AAAAAEiWeE_WKW4ORQxRzw
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments