Header Ads

Header ADS

ZAKAH SEHEMU YA 29

 

Assalam Alaykum Wa RahamatuLLAH Wa Barakatuh

*KUTOA ZAKAH*

=======🔹🔷🔹
=======

_SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA_

*Swadaqah*

*Kuwasaidia Wanyama*

```Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema kuwaambia Maswahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum):

"Mtu mmoja aliyekuwa akitembea, alishikwa na kiu, akaona kisima mbele yake, akateremka na kunywa maji ndani yake kisha akatoka. Alipokuwa akitoka alimuona mbwa akihema kwa kiu. Yule mtu akasema; "Bila shaka mbwa huyu ameshikwa na kiu kama nilivyoshikwa mimi. Akateremka (tena) kisimani, akajaza maji kiatu chake, kisha akamshika kichwa chake mbwa yule na kumnywesha.

Akashukuriwa na Allaah na kughufuriwa".

Maswahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhu) wakasema:

"Hata katika wanyama tunapata thawabu?"

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:

"Katika kila chenye uhai mna thawabu".

Al-Bukhaariy```

 
*Swadaqatun Jaariyah*

```Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

"Mwanaadamu anapokufa, amali zake zote zinakatika isipokuwa tatu. Swadaqatun Jaariyah (Swadaqah inayoendela), au elimu yenye kunufaisha watu, au mtoto mwema anayemuombea".

[Ahmad na Muslim]```
 
*Kushukuru*

```Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

"Atakayekufanyieni wema mlipeni, na ikiwa hamna cha kumlipa, basi muombeeni dua mpaka muhisi kuwa mumemlipa".

[Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy]

Imesimuliwa na Imaam Ahmad kutoka kwa Al-Ash’ath bin Qays kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

"Hamshukuru Allaah yule asiyewashukuru watu."

Ahmad

Na akasema:

"Aliyetendewa jema, akasema kumwambia aliyemtendea: “Jazaaka Allaahu khayran', (Allaah  Akujaze khayr), huyo amekwisha shukuru kama inavyotakikana".

Itaendelea In shaa Allah```

*+97433799776*
*RAUDHWATUL ILM*

*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵*

https://t.me/joinchat/AAAAAEiWeE_WKW4ORQxRzw

QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566

TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾

websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/

Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks

Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah

Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE

telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk

YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A

 

No comments

Powered by Blogger.