ZAKAH SEHEMU YA10
Assalam Alaykum Wa RahamatuLLAH Wa Barakatuh
*KUTOA ZAKAH*
=======🔹🔷🔹
=======
_SEHEMU YA KUMI_
*Mtoto Na Mpungufu Wa Akili*
```▶Inamuwajibikia aliyekabidhiwa mali ya yatima au ya mtu mwenye upungufu wa akili kuitolea Zakaah mali hiyo ikifikia kiwango chake.
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amru (Radhwiya Allaahu ‘anhu), anasema kuwa; Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"Mwenye kumlea yatima mwenye mali, basi aifanyie biashara mali hiyo na asiiache mpaka ikamalizika kwa kuliwa na Swadaqah (Zakaah)".
Anasema Shaykh Sayyid Saabiq katika Fiqhis Sunnah kuwa; Isnadi yake ina udhaifu ndani yake. Akaendelea kusema:
“Anasema Al-Haafidh kuwa Hadiyth hii ina ushahidi kuwa ni 'Mursal' iliyorushwa moja kwa moja mpaka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) bila ya kutaja isnadi. Ama Imaam Ash-Shaafi’iy ameikubali (hadithi hii) kwa sababu zipo Hadiyth nyingi zinazoelezea juu ya kuwajibika kwa Zakaah katika mali yoyote ile. Anasema Imaam At-Tirmidhiy kuwa wanavyuoni wamekhitalifiana juu ya kuwajibika kuitolea Zakaah mali ya yatima,” amemaliza kusema Shaykh Sayyid Saabiq.```
*Watts app - +97433799776*
*RAUDHWATUL ILM*
*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LIÑK IFUATAYO⤵*
https://t.me/joinchat/AAAAAEiWeE_WKW4ORQxRzw
WASAMBAZAJI
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
No comments