ZAKAH SEHEMU YA11
Assalam Alaykum Wa RahmatuLLLAH Wa Barakatuh
*KUTOA ZAKAH*
=========🔹🔷🔹
=========
_SEHEMU YA KUMI NA MOJA_
*Mwenye Deni*
```▶Mwenye kumiliki kiwango kinachomwajibisha kutoka Zakaah, na wakati huo huo anadaiwa, kwanza anatoa kiasi cha deni analodaiwa, kisha anailipia Zakaah mali iliyobaki ikiwa bado inafikia kiwango cha kutolewa Zakaah. Ama ikiwa mali iliyobaki haifikii kiwango, basi hatoi Zakaah, kwa sababu wakati huo anahesabiwa kuwa ni mtu fakiri, na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:
"Hatoi Swadaqah (Zakaah) isipokuwa mtu tajiri".
[Ahmad]
Na amesema:
"Ichukuliwa (mali ya Zakaah) kutoka kwa matajiri wao na kurudishiwa mafakiri wao".```
__________________________________
*Aliyefariki*
```▶Anasema Sayyid Saabiq katika Fiqhis Sunnah kuwa, katika madhehebu ya Maimaam Ash-Shaafi’iy na Ahmad na Abuu Thawr, ni kuwa mtu akifarki na akaacha deni la Zakaah, basi inawajibika katika mali yake kwanza kutolewa deni la Zakaah, tena iwe kabla ya kutimizwa wasia alioacha na kabla ya urithi kugawiwa.
Allaah Anasema:
مِن بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصِي بِهَا أَوْ دَيْنٍ
"Baada ya kutoa aliyoyausia au kulipa deni".
[An-Nisaa: 11]
Na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"Deni la Allaah linastahiki zaidi kulipwa".
Na Zakaah ni deni la Allaah.
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa amesema:
“Mtu mmoja alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:
"Mama yangu amefariki na anadaiwa saumu ya mwezi mzima, je nimlipie?"
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza:
"Mama yako angelikuwa na deni ungemlipia?"
Akasema:
"Ndiyo, ningemlipia".
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia:
"Basi deni la Allaah linastahiki zaidi kulipwa".
[Al-Bukhaariy na Muslim]```
*Niyah*
```▶Zakaah ni ‘Ibaadah, na kwa ajili hiyo kutia Niyyah ni jambo muhimu kama ilivyo katika ‘Ibaadah yoyote ile. Na Niyah ni kitu cha moyoni na hakina uhusiano na ulimi, na kusudi lake ni kuwa mtu anapotoa Zakaah akusudie kuitoa kwa ajili ya Allaah.
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"Hakika ya amali yoyote ni kutokana na Niyyah, na mtu hulipwa kutokana na Niyyah yake".
Itaendelea In shaa Allah```
*Watts app -+97433799776*
*RAUDHWATUL ILM*
*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LIÑK IFUATAYO⤵*
https://t.me/joinchat/AAAAAEiWeE_WKW4ORQxRzw
WASAMBAZAJI
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
No comments