Header Ads

Header ADS

ZAKAH SEHEMU YA 22

 Assalam Alaykum Wa RahamatuLLAH Wa Barakatuh



*KUTOA ZAKAH*


========🔹🔷🔹

========


_SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI_


*Zakaah Ya Wanyama Wa Kufugwa*

 

```Wanyama wanaofugwa wanalazimika kutolewa Zakaah kwa masharti yafuatayo:


1.  Lazima watimie Niswaab


2.  Wakamilishe mwaka


3.  Wawe wanyama wa kufugwa.


Wanyama wasiokuwa wa kufugwa kama vile wa kupandwa au wanaotumiwa kwa kubeba mizigo au kwa kilimo n.k. Hawa hawatolewi Zakaah.


Wanyama wanaotolewa Zakaah ni Ngamia, Ng'ombe, Mbuzi na Kondoo.```


 

*Zakaah Ya Ngamia*



```Ngamia hawatolewi Zakaah mpaka watimie watano. Wakitimia watano wa kufugwa hadi tisa na kutimiza mwaka chini ya milki ya mtu, basi atawatolea mbuzi mmoja.


Wakitimia ngamia 10 mpaka 14 atawatolea mbuzi wawili.


Na hivyo hivyo kila wakizidi ngamia watano ataongeza mbuzi mmoja.


Wakitimia ngamia 25 mpaka 35 atatoa mtoto wa ngamia jike aliyekamilisha mwaka na kuingia mwaka wa pili au mtoto wa ngamia dume aliyekamilisha mwaka wa 2 na anaingia wa 3.


Kuanzia ngamia 36 mpaka 45 atatoa mtoto wa ngamia jike aliyekamilisha miaka 2 na keshaingia wa 3.


Kuanzia ngamia 46 mpaka 60 atatoa mtoto wa ngamia jike aliyekamilisha miaka 3 na kuingia wa 4.


Kuanzia ngamia 61 mpaka 75 atatoa mtoto wa ngamia jike aliyekamilisha miaka 4 na kuingia mwaka wa 5.


Kuanzia ngamia 76 mpaka 90 atatoa watoto wa ngamia wawili jike waliokamilisha miaka miwili na kuingia wa tatu.


Kuanzia ngamia 91 mpaka 120 atatoa watoto wa ngamia wa kike wawili waliotimia miaka 3 na kuingia mwaka wa 4.


 


Wakizidi kuliko hapo, basi katika kila ngamia 40 atatoa mtoto wa ngamia wa kike aliyekamilisha miaka 2 na kuingia wa 3. Na katika kila ngamia 50 waliozidi kuliko hapo atatoa mtoto wa ngami wa kike aliyekamilisha miaka 3 na kuingia wa nne.


 


Anasema Sayyid Saabiq katika Fiqhis Sunnah:


"Hawatolewi Zakaah ngamia dume ikiwa wapo wa kike, lakini anatolewa mtoto wa ngamia wa kiume aliyetimia miaka miwili na kuingia wa tatu ikiwa hajapatikana wa kike aliyekamilisha mwaka na kuingia wa pili.```


Itaendelea In shaa Allah

 

*Watts app - +97433799776*

*RAUDHWATUL ILM*


*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵*


 https://t.me/joinchat/AAAAAEiWeE_WKW4ORQxRzw


QURAN NA SUNNAH TZ 

WHATSAPP NO +255713849566 


TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾


websites.

http://qurannasunnahtz.blogspot.com/


Facebook page.

https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks


Instagram.

http://www.instagram.com/qurannasunnah


Whatsapp.

https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE


telegram.

https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk


YouTube

http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A



 

No comments

Powered by Blogger.