Header Ads

Header ADS

ZAKAH SEHEMU YA 23

 Assalam Alaykum Wa RahamatuLLAH Wa Barakatuh


*KUTOA ZAKAH*


=======🔹🔷🔹

=======


_SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU_


 *Zakaah Ya Ng’ombe*

 

```▶Ng'ombe hawatolewi Zakaah mpaka watimie 30 wa kufugwa. Wanapotimia 30 mpaka 39 wa kufugwa na kukamilisha mwaka, atatolewa ndama aliyekamilisha mwaka mmoja.


Wakitimia ng'ombe 40 mpaka 59 atatolewa ndama asiyepungua umri wa miaka miwili.


Wakitimia ng'ombe 60 mpaka 79 atatolewa ndama wawili wa mwaka mmoja.


Kutoka hapo, kila wakizidi ng'ombe 30, ataongeza kutoa ndama wa mwaka mmoja.


Na kila wakizidi ng'ombe 40 atawatolea ndama wa miaka miwili.```


 

*Zakaah Ya Mbuzi*


```Mbuzi hawatolewi Zakaah mpaka watimie 40, na wakitimia arubaini mpaka 120 wa kufugwa na kukamilisha mwaka kwa mwenye kuwamiliki, atawatolea mtoto wa mbuzi wa mwaka mmoja.


Hatowatolea tena mpaka wafikie idadi yao mbuzi 121.


Wakiongezeka na kutimia 121 mpaka 200, atawatolea mtoto wa miaka miwili.


Kuanzia mbuzi 201 mpaka 300 atawatolea kondoo watatu.


Wakizidi kuliko mbuzi 300, basi atawatolea kondoo mmoja katika kila mbuzi mia waliozidi.


Inaruhusiwa pia kutoa mbuzi badala ya kondoo.```


 

*Wanyama Wengine*

 


```Wanyama wengine wasiokuwa hawa kama vile farasi, nyumbu, punda na wengineo, hawatolewi Zakaah isipokuwa kama ni kwa ajili ya biashara.```


 

*Zakaah Ya Madini Ya Kale*

 

```Madini inayotolewa ardhini kama vile petroli, gesi, shaba, chuma n.k, hivi vyote havitolewi Zakaah, isipokuwa dhahabu na fedha tu na tushaelezea hapo mwanzo namna ya kutoa Zakaah yake. Ama vilivyobaki vinatolewa Zakaah ya biashara baada ya kuchimbuliwa au kutolewa na kuuzwa```


Itaendelea In shaa Allah


*+97433799776*

*RAUDHWATUL ILM*


*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵*


 https://t.me/joinchat/AAAAAEiWeE_WKW4ORQxRzw


QURAN NA SUNNAH TZ 

WHATSAPP NO +255713849566 


TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾


websites.

http://qurannasunnahtz.blogspot.com/


Facebook page.

https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks


Instagram.

http://www.instagram.com/qurannasunnah


Whatsapp.

https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE


telegram.

https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk


YouTube

http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A



 

No comments

Powered by Blogger.