TABIA NJEMA SEHEMU1
🌹 *_رياض الصالحين (SEH:1)_* 🌹
🌺 *_TABIA NJEMA_* 🌺
▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂
🔻 *_KUACHA TABIA YA UOMBAJI { OMBA OMBA }_*
→ Uombaji kwa baadhi ya watu imekuwa kama ni sehemu ya kujiengezea au kujipatia kipato chao kiasi ambacho mtu hata kama anayo rizki inayomtosheleza lakini lazima aombe ili aengeze katika kipato chake
‼ Tabia ya uombaji bila kuwa na dharura inatokana na jambo kuu moja :
① *_Mtu kutokukina / hatosheki / haridhiki na kile alichonacho_*
Wakati kuridhika na kukinai ni katika Tabia na mwenendo mwema kama mtume ﷺ anavyosema :
♻ " Utajiri si kuwa na mali nyingi , Bali utajiri ni utajiri wa nafsi " bukhari { 6446 } na Muslim { 1051 }
________
🔻 *_KUOMBA BILA YA DHARURA_* 🔻
→ Uislamu unakataza mtu Kuomba ovyo , au Kuomba bila kuwa na dharura :
♻ ▪️ قَالَ رَسُولَ اللَّه ﷺ :
💉 " Mwenye Kuomba watu kwa ajili yakujizidishia ( mali ) hakika yuwaomba kaa la moto , basi apunguze au azidishe " Muslim { 1041 }
♻ ✾ قال ابن العثيمين رحمه الله :
→ Hadithi hizi zimekuja katika kubainisha makemeo kwa yule mwenye kuwaomba watu bila dharura , .... Mwenye kuwaomba watu ili ajiengezee mali yake basi huyo anaomba kaa la moto , basi azidishe huko Kuomba au apunguze , akizidisha anajizidishia makaa na akipunguza anajipunguzia , na akiacha anajisalimisha / anajiepusha na kaa la moto ,
*_Na katika hili kuna dalili kuwa Anaeomba watu bila ya kuwa na haja ni katika madhambi makubwa_*
📜الـــمَــصــــــــــدر
🔍 شرح رياض الصالحين { ٢/٢٤٥ }
✍ *_Kwaio_* Tunapaswa kutosheka na kile ambacho Allah ameturuzuku nasio Kuomba OMBA wakati huna shida wala dharura yakufanya hivyo
Allah anajua zaidi
_*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵*_
https://t.me/joinchat/AAAAAEiWeE_WKW4ORQxRzw
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments