TABIA NJEMA SEHEMU 2
🌹 *_رياض الصالحين{ 2 }_*🌹
🌺 *_TABIA NJEMA_* 🌺
▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂
🔻 *_KUACHA DHULMA NA UBAGHILI_*
→ kwa masikitiko makubwa , waislamu wa leo tumejipamba na tabii hizi mbaya : *_Dhulma_* : watu wana dhulumiana na kuibiana mali zao kiasi ambacho hakuna tofauti baina ya vijana wa kiislamu na wasio waislamu : *_Ubaghili_* : leo hii uislamu hauendi mbele kwa sababu ya ubaghili wetu, mtu anaona tabu kutoa mali yake kwa ajili ya akhera yake
🔻 *_DHULMA_* 🔻
→ Dhulma ni kuwafanyia uadui wengine na Dhulma kubwa ni kumshirikisha Allah mtukufu kama anavyosema :
*_وَإِذْ قَالَ لُقْمَانُ لِابْنِهِ وَهُوَ يَعِظُهُ يَا بُنَيَّ لَا تُشْرِكْ بِاللَّهِ ۖ إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ_*
۞ Na Luqman alipo mwambia mwanawe kwa kumpa mawaidha: Ewe mwanangu! Usimshirikishe Allah. Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni dhulma iliyo kubwa. ۞
→ Ukiachilia Dhulma ambayo mtu anamfanyia mola wake kwa kumshirikisha , pia ipo Dhulma ambayo mwanaadamu anawafanyia viumbe wenziwe nayo Dhulma hii ipo ya aina mbili
➊ Kuwacha jambo la wajibu Kwao kuwafanyia
➋ Dhulma katika kuwafanyia uadui
Na mifano ipo mingi ya aina hizo mbili za Dhulma kama vile :
a} Kumpokonya mtu ardhi yake , au mali yake , au kujizidishia kiwanja katika ardhi ya mtu , kumuuzia MTU kitu ambacho Sio chako nk
b} kuwavunjia watu heshima zao iwe kwa kumtukana mtu , kumsema vibaya au kumsengenya
🔻 *_UBAGHILI_* 🔻
→ Ubaghili ni ile hali yakuzuia kile ambacho ni wajibu kwako kutoa , kutumia au kuchangia
Mwanaadamu anatakiwa atoe kile ambacho ni wajibu kutoa kama vile elimu , mali nk
♻ ▪️ قَالَ رَسُولَ اللَّه ﷺ :
→ " Ogopeni Dhulma , hakika Dhulma ni magiza siku ya kiama , na ogopeni Ubaghili , hakika Ubaghili uliwaangamiza waliokuwa Kabla yenu , uli wafanya wamwage damu zao na wakahalalisha walio haramishiwa " Muslim { 257)
Allah anajua zaidi
_*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵*_
https://t.me/joinchat/AAAAAEiWeE_WKW4ORQxRzw
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments