TABIA NJEMA SEHEMU YA 3
🌹 *_رياض الصالحين ( 3: SEH )_*🌹
🌺 *_TABIA NJEMA_* 🌺
▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂
🔻 *_KUSAIDIA NA KUWAPENDELEA WATU MAMBO YA KHERI_*
→ Katika Darsa iliopita tumesoma juu ya Tabia mbaya ya Ubaghili : na Ubaghili unatokana na mtu kutomtanguliza ndugu yake muislamu katika shida zake
Mtu yoyote ambae anawatanguliza wenziwe kuliko nafsi yake basi kamwe hawezi kuwa mbaghili Bali atatoa kadri ya uwezo wake ili kuwasaidia watu pindi wanapokutwa na matatizo
🔻 *_KUMTANGULIZA MWENZIO KULIKO NAFSI YAKO_* 🔻
→ Zimekuja dalili mbali mbali katika Quran na sunna , kubainisha kuwa watu wema ni wale ambao watawatanguliza na kuwapendelea wenzao kuliko nafsi zao :
(❶)
" Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa (Wahajiri), bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa." { 59:9 }
(❷) " Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa " [[ yani licha yakuwa wao chakula wanakipenda lakini wanajitolea kuwapa mayatima , masikini .. ]] { 76 : 8 }
📌● Licha ya kuwa uislamu unatutaka tuwafikirie wenzetu kuliko nafsi zetu lakini kuwapendelea huko kuna vigawanyo vyake
① Haifai / imekatazwa :
→ haifai kumpendelea au kumtanguliza mwengine kuliko nafsi yako katika mambo ambayo kwako ni wajibu kuyafanya
*_Mfano_* huwezi kumuamrisha Mwenzio akaswali kisha wewe umekaa tu Halafu unamwambia niombee dua Uko , au nenda kaswali Mim Nakutakia kheri
Mfano mwengine ambao wanavyuoni wameutoa : mfano una maji ni machache Halafu upo na Mwenzio na nyote hamna udhu : ukampa Mwenzio maji Halafu wewe ukatayamamu , hapa wanasema uitangulize nafsi yako kwa kutumia maji yako , Halafu yeye ndio atatayamam
② Inajuzu / inafaa
→ inajuzu kumtanguliza Mwenzio kuliko nafsi yako haswa katika mambo ambayo Sio ya kiibada
Ikitokezea kwa mfano unachakula na unanjaa lakini akatokea mtu ananjaa pia basi inaruhusika kuipendelea nafsi ya mwenzako kwa kumpa yeye
Au una pesa ushaipangia mahisabu lakini akaja Mwenzio anashida , basi unatakiwa umpe akakidhi haja zake nk
__________
✍ *_Kwa ufupi_* : uislamu unahimiza Tuache Ubaghili na tuwahurumie ndugu zetu ambao wana shida na matatizo
Ikitokea cha leo ushakijua , akaja mtu anashida basi usianze kufikiria kesho au keshokutwa utakula nin , Bali msaidie ndugu yako na Allah yupo pamoja na wanao mcha.
Allah anajua zaidi
_*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵*_
https://t.me/joinchat/AAAAAEiWeE_WKW4ORQxRzw
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments