TABIA NJEMA SEHEMU 4
🌹 *_رياض الصالحين (4 )_*🌹
🌺 *_TABIA NJEMA_* 🌺
▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂
🔻 *_KUSHIRIKIANA NA WATU_* 🔻
→ Wengi katika waislamu wa leo , tumeshindwa kujipamba na Tabia hii ya kutangamana / kushirikiana na watu katika mambo mbali mbali yanayotokea
Tumeipa kipao mbele dunia na harakati zake kiasi ambacho kila mda mtu yupo busy na mambo yake au shughuli zake , au biashara zake bila kushiriki chochote kinachotokea katika familia au jamii anayo ishi
Uislamu umetuhimiza kushirikiana na watu na kutangamana nao vizuri katika :
① Vikao vyenye kheri
② kuzuru na kutembelea wagonjwa
→ Leo hii mtu ndugu yake au jamaa yake anaumwa lakini anashindwa kutumia hata dakika 10 kwenda kumtembelea , badala yake anashuhulika zaidi na harakati au biashara zake
③ Kuhudhuria mazishi
④ kuwafariji wenye shida
⑤ kutowaudhi watu
________
Zimekuja dalili mbali mbali katika Quran na sunna , kubainisha kuwa tunatakiwa tutangamane na watu vizuri
🔻 *_USHAHIDI_* 🔻
(❶) " Na saidianeni katika wema na uchamungu "
(❷) mtume ﷺ ametuamrisha kumzuru mgonjwa , kufata jeneza , kumuombea dua aliepiga chafya , kumfanyia alieapa lile alitakalo , kumnusuru aliedhulumiwa , kumuitikia aliealika na kueneza salamu " Bukhari { 1239 } , Muslim { 2066 }
(❷) " Haki ya muislamu juu ya muislamu ni tano : kurudisha salamu , kumzuru mgonjwa , kufwata jeneza , kuitikia mualiko na kumuombea dua aliepiga chafya " Bukhari { 1240 } , Muslim { 2162 }
(❸) " wazuruni wagonjwa , mlisheni mwenye njaa na muwache huru mateka " Bukhari { 6502 }
_________
✍ *_Kwa ufupi_* : muislamu hutakiwi ujitenge au uoneshe ubinafsi , Bali ni katika Tabia njema kushirikiana na watu katika Mas-ala mbali mbali yenye kheri ambayo yanatokea iwe katika familia au jamii ilio kuzunguka
Itaendelea In shaa Allah
_*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵*_
https://t.me/joinchat/AAAAAEiWeE_WKW4ORQxRzw
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments