TABIA NJEMA SEHEMU YA 4 NYIONGEZA
📚📚
📚
🌹 _*NYONGEZA*_🌹
Katika post hio juu tumeona kuwa tunatakiwa tushiriki katika furaha , matatizo au majanga ambayo yanatokea katika jamii zetu
👉 kuhusiana na mualiko Tayari tushasoma katika Darsa ya ndoa kuwa unapoalikwa unatakiwa uitikie mualiko na kama umedharurika basi LAZIMA utoe taarifa kwa aliekualika kuwa Sito wahi
👆 Sio binaadamu wewe kila ukialikwa Huendi tena huna sababu yoyote ya msingi Bali biashara zako tu eti zimekuzonga
Hapana : uislamu unakutaka ushirikiane na watu katika mambo yao mbali mbali
💉 Pia tunatakiwa tushiriki katika kuwakagua wagonjwa , iwe ni ndugu au marafiki au majirani zetu nk
Tuanze na kipengele hichi kwa kuangalia faida mbali mbali na utaratibu wa kiislamu katika kadhia hii ya kwenda kumtizama au kumkagua mgonjwa 👇
1⃣
🔻 *_ADABU ZA KWENDA KUMKAGUA MGONJWA_* 🔻
➊ Kuweka niya kuwa unafanya hivyo kwa kutekeleza amri ya mtume ﷺ
➋ Pia uweke azma kuwa unafanya hivyo kwa kumfanyia wema uyo mgonjwa , kwani mgonjwa anapotembelewa hujisikia raha na kufarijika
➌ Usikae muda mrefu kwa mgonjwa kwani kufanya hivyo utamchosha na ilhali anatakiwa apate muda mrefu waku pumzika
➍ Utumie nafasi hio kumfahamisha mgonjwa yale ambayo yanamanufaa kwake , kama vile alete toba kwa wingi nk
➎ Pia kama wewe una elimu : na mgonjwa anapata tabu katika kutawadha au namna ya kuswali basi unatakiwa umueleweshe njia rahisi za kufanya kwa mujibu wa uislamu ulivyo fanyia wepesi
➏ Pia angalia maslahi ya wewe kukaa sana kwa mgonjwa :
Ukiona hakuna maslahi au udhuru Huo basi hutakiwi ukae muda mrefu , Bali mkague uende zako
Ama Ukiona uwepo wako wewe ndio unamfanya mgonjwa afarijike basi unaweza kukaa kwa kadri ya hali
📚 شرح رياض الصالحين { ٣/٤٠ }
_________
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments