NDOA SEHEMU YA 12
*Assalaam A'laykumu Wa Rahmatul LLAAHI Wa Barakaatuh*
🛑 *SIKU YA MWANZO* 🛑
*YA NDOA*
*ليلة الزّفاف*
```SEHEMU YA KUMI NA MBILI```
============🔹🔷🔹=============
*Siku hii ndio siku ya mwanzo ya ndoa*, ni siku ambayo yenye athari kubwa katika maisha ya Mwanamme Bwana harusi na Mwanamke Bibi harusi kwa matokeo yoyote ya matendo ya siku hii.
Ni vizuri na muhimu sana kwa siku hii ya leo kwa mume kumfanyia upole mkewe na kuzungumza nae na kumzoea na kumuondoa khofu, na vizuri washauriwe wanandoa hawa wapya kuwa na utulivu na wasiwe na pupa yoyote ya jambo, maisha ni marefu na yana wasaa na siku zinakuja hakuna haja ya haraka.
Katika siku hii muhimu sana kwa wanandoa hawa ni vizuri kuchunga miiko ifuatayo :-
5⃣ *Adabu za Kuingiliana* ( *أدب الجماع* )
Imepokewa vile vile kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhiya ALLAAHU 'anhu) kuwa Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) amesema:
*إذا جامع أحدكم أهله فليصدقها , فإذا قضى حاجته قبل أن تقضي حاجتها فلا يعجلها حتى تقضي حاجته*
*“Atakapomuingilia mmoja wenu mkewe na amsadikishe (yaani wote wafikie kilele cha ladha ya kitendo cha ndoa), atakapomaliza haja yake kabla ya mke wake kumaliza ya kwake basi asifanye haraka hadi mke wake nae amalize haja yake.”* ( Abu Ya'ala )
Tunajifunza katika hadithi hii mafundisho ya kisheria yenye kumtaka mume amsubiri mke wake nae amalize haja yake, amshibishe na afikie kilele kama alivyofika yeye. Mafundisho haya ya Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) yanatufundisha kujali hisia za mwanamke na kuziheshimu.
6⃣ *Kuoga baina ya Matendo ya Ndoa* ( *الإغتسال بين الجماع* )
'Umar (Radhiya ALLAAHU 'anhu) amesema kuwa Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) amesema: *“Atakayemuingilia mke wake kisha akataka kurejea tena katika tendo la ndoa na asafishe tupu yake.”* (Atw-Twabaraaniy).
Kadhalika imesimuliwa toka kwa Abu Rafi kuwa Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) siku moja aliwazungukia wake zake, akioga kwa huyu na akioga kwa yule. Nikamwambia (Abu Rafi): *Ee, Mtume wa ALLAAH, je, huwezi kujaalia josho moja? Akasema Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) : “Hivi ni bora, vizuri zaidi na safi zaidi.”* (Abu Daawuwd na Ibn Maajah). Katika hadithi nyingine Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) anasema:
*إذا أتى أحدكم أهله ثم أراد أن يعود , فليتوضأ بينهما وضوءه للصّلاة*
*“Atakayemuingilia mkewe kisha akataka kurudi tena (katika tendo la tendo) na atawadhe baina ya matendo mawili wudhuu wa Swalah.”*
(Muslim, Abu Daawuwd, An-Nasaaiy na Ibn Maajah)
Katika kuchukua wudhuu, kukosha au kuoga ni katika jumla ya kuchangamsha mwili na kuziibua upya nguvu za kiwiliwili. Na si hivyo tu kunahakikisha usafi katika tendo la ndoa (sexual Hygiene).
Itaendelea tena In Shaa ALLAAH
*☎+97433799776*
*NDOA KATIKA UISLAM*
*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵*
https://t.me/joinchat/AAAAAEyebkF4FS9BJV3hkA
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments