ZAKAH SEHEMU YA 34
Assalam Alaykum Wa RahamatuLLAH Wa Barakatuh
=======🔹🔷🔹
=======
_SEHEMU YA THALATHINI NA NNE_
*Wanaostahiki Zakaah*
*Katika Kugomboa*
```Uislam umeijaalia ‘Ibaadah hii ya kuwagomboa mateka na watumwa kuwa ni kitendo kinachompatia mtu thawabu nyingi sana na kumuingiza katika Pepo za Allaah Subhanaahu wa Ta’ala.
Kutoka kwa Al-Barra-a (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema:
"Mtu mmoja alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kumwambia:
"Nijulishe juu ya amali (njema) itakayonikurubisha na Pepo na kunibaidisha na Moto".
Akasema:
"Waachie huru watu na wagomboe watumwa".
Akauliza (tena):
"Ewe Mtume wa Allaah, si yote hayo yanabeba maana moja tu?"
Akasema:
"La, (sivyo), 'kuwaachia huru' ni kujihusisha peke yako katika kuwaacha huru, na 'kuwagomboa' ni kusaidia katika kulipa thamani ya kuwagomboa".
[Ahmad na Ad-Daaraqutniy].
Wakati ule ilikuwa mtumwa anaweza kuandikiana na kukubaliana kuwa atakapoweza kulipa malipo fulani katika muda fulani, ataachwa huru. Kwa hivyo Waislam walitakiwa wawasaidie watu wa aina hiyo kwa kuwalipia kiasi hicho ili waweze kujigomboa.```
*📚Kumsaidia Mwenye Deni*
```Hawa ni wale wenye madeni makubwa wakashindwa kuyalipa kutokana na kula hasara katika biashara zao nk. Sharti madeni hayo yawe katika mambo ya halali au yatokane na maasi aliyotubu nayo mtu huyo.
Imepokelewa kutoka kwa MaImaam Ahmad na Abuu Daawuwd na Ibn Maajah na At-Tirmidhiy, kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema:
"Mas-alah (ya kuwasaidia wenye madeni), hayawi halali isipokuwa katika mambo matatu; aliye fakiri sana, au mwenye deni zito sana, au mwenye kudaiwa damu (ya diya - fidiya).”
(Huyu ni mtu aliyejikuta amebebeshwa deni la diya kutokana na ndugu yake au jamaa yake aliyeuwa kwa bahati mbaya. Ikiwa hajalipa diya hiyo, basi ndugu yake huyo au jamaa yake atauliwa kwa ajili ya kulipa kisasi)
Itaendelea In shaa Allah```
*+97433799776*
*RAUDHWATUL ILM*
*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵*
https://t.me/joinchat/AAAAAEiWeE_WKW4ORQxRzw
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments