NDOA SEHEMU YA 11
*Assalaam A'laykumu Wa Rahmatul LLAAHI Wa Barakaatuh*
🛑 *SIKU YA MWANZO* 🛑
*YA NDOA*
*ليلة الزّفاف*
```SEHEMU YA KUMI```
============🔹🔷🔹=============
*Siku hii ndio siku ya mwanzo ya ndoa*, ni siku ambayo yenye athari kubwa katika maisha ya Mwanamme Bwana harusi na Mwanamke Bibi harusi kwa matokeo yoyote ya matendo ya siku hii.
Ni vizuri na muhimu sana kwa siku hii ya leo kwa mume kumfanyia upole mkewe na kuzungumza nae na kumzoea na kumuondoa khofu, na vizuri washauriwe wanandoa hawa wapya kuwa na utulivu na wasiwe na pupa yoyote ya jambo, maisha ni marefu na yana wasaa na siku zinakuja hakuna haja ya haraka.
Katika siku hii muhimu sana kwa wanandoa hawa ni vizuri kuchunga miiko ifuatayo :-
2⃣ *Swalah ya Sunnah kwa Wanandoa*( *سنّة صلاة الزّواج*)
*Usiku wa mwanzo* wa Mume na Mke si kwa ajili tu ya kujifurahisha pekee na raha ya kuingiliana bali ni lazima kutekeleza amri za Dini na katika hayo ni Swalah. Amesema Mtume (Swalla ALLAAH 'alayhi wa sallam) :-
*إذا تزوّج أحدكم فكانت ليلة البناء فليصلّ ركعتين , وليأمرها أن تصليّ خلفه , فإنّ الله جاعل في البيت خيرا*
*“Atakapooa mmoja wenu na ikawa ni siku ya mjengo na aswali rakaa mbili na amuamuru mke wake aswali nyuma yake, kwani ALLAAH Atajaalia katika nyumba hiyo kheri.”*
(Imepokewa na al-Bazaar kama ilivyo katika kashfu al-Astaar)
Mtume Amesema juu yake Swalah na amani:
*إذا دخلت المرأة على زوجها يقوم الرّجل فتقوم من خلفه فيصلّيان ركعتين ويقول : اللهم بارك لي في أهلي وبارك لأهلي فيّ , اللهم ارزقهم مني , وارزقني منهم , اللهم اجمع بيننا ما جمعت في خير , وفرّق بيننا إذا فرّقت إلى خير*
*“Atakapoingia mwanamke kwa mumewe, atasimama mwanamme na mwanamke atasimama nyuma yake, na wataswali rakaa mbili na atasema: Ee ALLAAH! Nibarikie mimi kwa ahli zangu na uwabariki kwangu ahli zangu*, *ee ALLAAH! Waruzuku wao kwangu na uniruzuku mimi kwao*, *ee ALLAAH!* *Tuunganishe mimi na mke wangu katika muunganisho wa kheri,* *na Utufarikishe*
*baina yetu kwa kheri* *pindi Utakapotufarikisha*.”
(Al-Bukhaariy na Muslim)
Itaendelea In Shaa Allah
*☎+97433799776*
*NDOA KATIKA UISLAM*
*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵*
https://t.me/joinchat/AAAAAEyebkF4FS9BJV3hkA
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments