NDOA SEHEMU YA 10
*Assalaam A'laykumu Wa Rahmatul LLAAHI Wa Barakaatuh*
Na'am tunaendelea na Darasa letu la Ndoa tukiwa bado tunaangazia mambo muhimu wanayotakiwa kuyazingatia Wana ndoa katika siku hii ya kwanza
🛑 *SIKU YA MWANZO* 🛑
*YA NDOA*
*ليلة الزّفاف*
```SEHEMU YA KUMI NA MOJA```
============🔹🔷🔹=============
*Siku hii ndio siku ya mwanzo ya ndoa*, ni siku ambayo yenye athari kubwa katika maisha ya Mwanamme Bwana harusi na Mwanamke Bibi harusi kwa matokeo yoyote ya matendo ya siku hii.
Ni vizuri na muhimu sana kwa siku hii ya leo kwa mume kumfanyia upole mkewe na kuzungumza nae na kumzoea na kumuondoa khofu, na vizuri washauriwe wanandoa hawa wapya kuwa na utulivu na wasiwe na pupa yoyote ya jambo, maisha ni marefu na yana wasaa na siku zinakuja hakuna haja ya haraka.
Katika siku hii muhimu sana kwa wanandoa hawa ni vizuri kuchunga miiko ifuatayo tulikwisha ona jambo la *kwanza* na la *pili* sasa tunaendelea kuona jambo la *tatu* na la *nne* :-
3⃣ *Kinachosemwa Unapomwingilia Mkeo*( *ما يقال عند الجماع*)
*Mume anaomba* anapomuingilia mkewe kwa du'aa aliyofundisha Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) :-
*بسم الله اللهّم جنّبنا الشيطان وجنّب الشيطان ما رزقتنا*
*“BismiLLaah, Ee ALLAAH, tuepushie sheitani na Umuepushe kwa kile Utakachoturuzuku.”* (Al-Bukhaariy na Muslim)
4⃣ *Malipo ya Kuingiliana* ( *ثواب الجماع*)
*Katika kuingiliana* hakupatikani kwa raha peke yake bali kunabeba ndani yake malipo mtu anayolipwa na ALLAAH (Subhaanahu wa Ta'ala) katika kufanya hivyo na mke wake au mume wake, amesema Abu Dharr (Radhiya ALLAAHU 'anhu) :
*“Hakika watu katika Maswahaba walimwambia Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) : *Ee Mtume wa ALLAAH wameondoka wenye uwezo (ahlu duthuur) na malipo yote, huswali kama tunavyosali, hufunga kama tunavyofunga, na hutoa sadaka katika bora ya mali zao*. Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) akawaambia, *“Je, ALLAAH Hakuwajaalia katika ya kutoa sadaka? Hakika katika kila tasbiyh (SUBHAANA-ALLAAH) ni sadaka. Na katika kila takbiyr (ALLAAHU AKBAR ) ni sadaka, na kila tahliyl (LA ILAAHA ILLA ALLAAH) ni sadaka. Na kila tahmiid (ALHAMDULILLAAH) ni sadaka. Kuamrisha mema ni sadaka na kukataza maovu ni sadaka vile vile na kumuingilia mkeo ni sadaka.”* Wakasema Maswahaba na je, katika kupata raha binafsi mmoja wetu analipwa??!. Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) akasema: *“Je, mnaonaje lau mtu huyo angeingiza (tupu yake) katika haramu, je, ingelikuwa ni shari juu yake (ya madhambi, maradhi, adhabu)?,* wakasema: *ndio*. Akasema Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) : *“Hivyo ndivyo atakapoweka (tupu yake) katika halali atalipwa.”* (Muslim)
In Shaa ALLAAH itaendelea tena baadaye In Shaa ALLAAH Kwakuona Mambo mengi zaidi yanayotakiwa kufanywa siku ya mwanzo katika ndoa
*☎+97433799776*
*NDOA KATIKA UISLAM*
*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵*
https://t.me/joinchat/AAAAAEyebkF4FS9BJV3hkA
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments