Header Ads

Header ADS

NDOA SEHEMU YA 9

 *Assalaam A'laykumu Wa Rahmatul LLAAHI Wa Barakaatuh*

 

Sifa zote njema Anastahiki ALLAAH Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla ALLAAHU ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya ALLAAHU ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. 


Na'am tunaendelea na Darsa


🛑 *SIKU YA MWANZO* 🛑

                          *YA NDOA* 

                                  *ليلة الزّفاف* 

                 ```SEHEMU YA TISA```

============🔹🔷🔹=============

*Siku hii ndio siku ya mwanzo ya ndoa*, ni siku ambayo yenye athari kubwa katika maisha ya Mwanamme Bwana harusi na Mwanamke Bibi harusi kwa matokeo yoyote ya matendo ya siku hii.

 

Ni vizuri na muhimu sana kwa siku hii ya leo kwa mume kumfanyia upole mkewe na kuzungumza nae na kumzoea na kumuondoa khofu, na vizuri washauriwe wanandoa hawa wapya kuwa na utulivu na wasiwe na pupa yoyote ya jambo, maisha ni marefu na yana wasaa na siku zinakuja hakuna haja ya haraka.

 

Katika siku hii muhimu sana kwa wanandoa hawa ni vizuri kuchunga miiko ifuatayo :-


1⃣ *Kumfanyia Upole na Kumlainisha Mkeo* ( *ملاطفة الزوجة* )

Mume anapoingia kwa mke wake katika siku hii muhimu katika maisha ya ndoa mara nyingi hisia za khofu na wasiwasi za mwanamke zinakuwa juu, hivyo basi ni juu ya mwanamme kukaa nae kwa upole na kumbembeleza hadi nae ajihisi anaanza kuzoea hali hiyo na kupunguza khofu na wasiwasi aliokuwa nao juu yako. Hekima itumike, ugomvi, matusi au kupiga si mahali pake kabisa, na sio lazima kumuingilia usiku ule ule, unaweza kusubiri hadi asubuhi au hata siku ya pili, mara nyingi mwenye pupa huwa anakosea na matokeo yake yanakuwa ni mabaya (na yenye kudumu katika maisha mazima ya ndoa yenu).

 

Imepokewa kutoka kwa Asmaa bint Yaziyd bin as-Sakan amesema: *“Nilimuendea Bibi 'Aaishah (Radhiya ALLAAHU 'anha) hali ya kuwa amejipamba kwa ajili ya Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) nikamuondoa khofu. Baada ya muda kidogo Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) akaja pembeni yake na kikombe cha maziwa, akayanywa kidogo kisha akampa Bibi 'Aaishah nae akateremsha kichwa chake kwa kuona haya. (Asmaa) nikamnyanyua ('Aaishah), nikamwambia: chukua kutoka kwa mkono wa Mtume wa ALLAAH. ('Aaishah) Akachukua na kuyanywa, kisha (Mtume (Swalla ALLAAHU 'alayhi wa sallam) akamwambia, “Wape marafiki zako wa umri wako.”* (Ahmad)

 

Na si neno kwa mke kumkatalia kidogo mumewe kwani katika hilo mtu husisimkwa, na hujitayarisha, na kunapelekea kumjali zaidi na kumtaka. Na kunanasihiwa kwa wanandoa kuwa ni vizuri wakavua nguo zao zote kama vile mshairi anavyosema:-

 

*Na tahadhari kuingiliana kunako nguo*

*Kwani huo ni ujahili usiokuwa na shaka!*

*Bali kila mlicho nacho,* *ee, rafiki yangu mkivue*

*Na uwe ni mchezaji nae ili asifadhaike*.

 

Ni Sunnah mume kusema anapoingia kwa mkewe siku ya mwanzo:-

        

  *اللهّم إني أسألك من خيرها وخير ما جبلته وأ عوذ بك من شرها وشّر ما جبلتها عليه*

 

*“Ee, ALLAAH nakuomba kheri yake na kheri aliyokuja nayo na uniepushe na shari yake na shari aliyokuja nayo.”* (Abu Daawuwd na Ibn Maajah)

 

Du'aa kama hii hutuliza hisia za mwanamke na Nafsi yake na hukaribisha baraka, na huenda kwa hayo ALLAAH Akajaalia baraka katika usiku huu.


In Shaa ALLAAH itaendelea 


*NDOA KATIKA UISLAM*


*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵*


https://t.me/joinchat/AAAAAEyebkF4FS9BJV3hkA


QURAN NA SUNNAH TZ 

WHATSAPP NO +255713849566 


TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾


websites.

http://qurannasunnahtz.blogspot.com/


Facebook page.

https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks


Instagram.

http://www.instagram.com/qurannasunnah


Whatsapp.

https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE


telegram.

https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk


YouTube

http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A



 

No comments

Powered by Blogger.