Header Ads

Header ADS

NDOA SEHEMU YA 13

 *Assalam A'laykum Wa RahmatuLLAH Wa Barakaatuh*


🛑

🛑         *SIKU YA MWANZO*


        *YA NDOA - ليلة الزّفاف*


```SEHEMU YA KUMI NA TATU```

===========🔹🔷🔹

===========


 7⃣ *Adabu za Mtu na Ndugu za Mke Wake - أدب الرّجل مع أقارب زوجته*


Katika jumla ya adabu ya mtu na ndugu za mke wake ni kutokutaja maneno au kufanya vitendo vya aina yoyote ile vyenye kuashiria mapenzi ya chumbani kama kubusu na mfano wa hayo, na hii ni katika adabu ya kuishi nao. Imepokewa kutoka kwa 'Aliy bin Abi Twaalib (Radhiya Allaahu 'anhu) amesema: nilikuwa ni mtu mudhaa-a, nikiona haya kumuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kwa nafasi ya mtoto wake kwangu, nikamuomba Miqdaad aniulizie.


8⃣ *Kuharamisha Kuingilia Katika Tupu ya Nyuma -*

 *تحريم نكاح الدّبر*


Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:


نساؤكم حرث لكم فأتوا حرثكم أنى شئتم

*“ Wake zenu ni konde zenu, basi ziendeeni konde zenu mpendavyo.”  (Al-Baqarah: 223)*


 

Ilikuwa ni tabia ya Mayahudi wakisema: Mtu atakapomuingilia mke wake mbele lakini kwa upande wa nyuma basi atazaliwa mtoto akiwa ni kengeza; ikashuka Aayah hii: *“Wake zenu ni mashamba yenu.” (Muslim)*. Katika riwaya nyingine:


إن شاء مجبّية و إن شاء غير مجبّية غير أنّ ذلك في صمام واحد 


*“…na ukipenda ufanye staili ya kama anasujudu na ukipenda sivyo hivyo yote ni sawa sawa...” (Muslim: Hadithi 1435)*


Ilikuwa ni tabia ya Ahlul-Kitaab kutomuingilia mwanamke ila kiubavu na katika hali ya mwanamke kujistiri. Na ilikuwa tabia ya baadhi ya Answaar kuiga tabia zao hizo. Na wanaume wa ki-Quraysh walikuwa wamezowea kufanya mapenzi na wake zao vilivyo, wakistarehe nao kwa mbele, nyuma na kwa chali, (lakini bila ya kuwaingilia tupu zao za nyuma). Walipohamia Muhajirina Madiynah alioa mmoja wao mwanamke wa ki-Answaar; akataka kufanya nae mapenzi kwa mitindo waliyozoea (huko Makkah) akachukizwa mwanamke yule na hilo, na akasema: Hakika sisi tulikuwa tukiingiliwa kiubavu, fanya hivyo au niepuke; kisa chao kikaenea, zikamfikia habari Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na Allaah Akashusha:


نساؤكم حرث لكم

*“Wake zenu ni konde zenu…” (Abu Daawuwd)*


 


Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  akasema vile vile:


*“(Waingilieni wake zenu kwa mtindo wa) Kwa mbele au (kwa mtindo wa) kwa nyuma lakini epukeni dubur (utupu wa nyuma) na (kuwaingilia wakati wako) kwenye hedhi.” (At-Tirmidhiy)*


Itaendelea In Shaa Allah


*☎+97433799776*

*NDOA KATIKA UISLAM*


*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵"*


https://t.me/joinchat/AAAAAEyebkF4FS9BJV3hkA



QURAN NA SUNNAH TZ 

WHATSAPP NO +255713849566 


TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾


websites.

http://qurannasunnahtz.blogspot.com/


Facebook page.

https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks


Instagram.

http://www.instagram.com/qurannasunnah


Whatsapp.

https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE


telegram.

https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk


YouTube

http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A



 

No comments

Powered by Blogger.