ZAKAH SEHEMU YA 37
Assalam Alaykum Wa RahamatuLLAH WA Barakatuh
*KUTOA ZAKAH*
=======🔹🔷🔹
=======
_SEHEMU YA THALATHINI NA SABA_
*Watu Wema*
```Zakaah anapewa Muislam anayeistahiki akiwa Muislam huyo ni mtu mwema au mtu asi, isipokuwa mtu asi hapewi katika mali ya Zakaah ikiwa itajulikana kwa uhakika kuwa atakuja kuitumia mali hiyo katika kuuendeleza uasi wake.
Ikijulikana kwa uhakika kuwa ataitumia mali hiyo katika kumuasi Mwenyezi Mungu, basi mtu huyo atanyimwa, ama ikiwa hayajulikani hayo, au ikijulikana kuwa ataitumia mali hiyo katika shida zake, basi hapo atapewa.
Hata hivyo ni bora kwa mtoaji Zakaah aihusishe mali hiyo kwa kuwapa watu wema au maulamaa wanaostahiki wanaoifayia kazi elimu yao, kwani Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
"Walisheni chakula chenu wachaMungu na mnaowajuwa katika walioamini (kweli)".
Ahmad
Anasema Ibn Taymiyah:
"Asiyeswali hapewi katika mali ya Zakaah mpaka pale atakapotubu akawa anaswali."
Anasema Sayyid Saabiq:
"Katika kundi hilo wanaingia pia wale wanaomuasi Mwenyezi Mungu bila kujali wala kuona haya, na kuendelea kuzama katika maasi huku nyoyo zao zikiwa ziAsh-Shaafi’iysidika na dhamiri zao zimekwisha haribika".
Hawa hawapewi katika mali ya Zakaah isipokuwa kama Zakaah hiyo itawasaidia katika kuwaongoza mwongozo ulio sahihi au itawasaidia katika kutoka hali yao hiyo.
Itaendelea In shaa Allah```
*+97433799776*
*RAUDHWATUL ILM*
*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵*
https://t.me/joinchat/AAAAAEiWeE_WKW4ORQxRzw
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments