SWALA YA MGOJWA SEHEMU YA 1
: ♻Assalam alaykum warahamatullah wabarakatuh
*Swalah ya Mgonjwa*
📚📚
📚
1⃣
*VIPI ATASWALI MGONJWA*
↩ kwanza ni wajibu kwa mgonjwa au mtu mwengine kuswali hali amesimama kwani kusimama ni nguzo katika nguzo za swala , Allah anasema :
📙 حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّهِ قَانِتِينَ
Zilindeni Sala, na khasa Sala ya katikati, na simameni kwa ajili ya Allah nanyi ni wenye ku (kunyenyekea).📙
{ البقرة : ٢٣٨ }
↩ Ama tukija kwa mgonjwa basi ni wajibu pia kwake kusimama , Hata kama ataweza kusimamia kitu kama fimbo au ukuta basi atatakiwa asimame
{ مجموع فتاوى بن صالح بن العثيمين : ١٥/٢٢٩ }
↩ Lakini wamekubaliana wanavyuoni kuwa mgonjwa kama Hawezi kusimama basi ataswali kwa kukaa na Hayo yanatokana na kauli ya mtume salallahu alayhi wasallam aliposema :
📗swali umesimama , kama huwezi , kwa kukaa .... 📗
{ اخرجه البخاري : ١١١٧}
↩ Lakini swali lakujiuliza utaswali vipi kwa kukaaa ??
Mtu atakaa kama vile ambavyo anavyokaa atahiyatu yakwanza (muftarisha) hivi Ndoivyo mtu atakavyokaa kama hawezi kuswali kwa kusimama
{ فقه السنة للنساء : ١٠٦ }
↩ kwa ufupi mtu atakaa mkao wowote ambao umewekwa na unakubalika katika sheria lakini lililobora akae mutarabbia (kama wanavyokaa watoto wa madrasa ) katika sehemu za kismamo na akae muftarisha (kile kikao cha attahiyatu ) katika sehemu zote zile za vikao
{ توضيح الاحكام :٢/١٦٩ }
↩ Ama ikiwa mgonjwa hawezi kukaa na hawezi kuswali kwa kukaa basi ataswali kwa kulala , na atalalia ubavu wakulia na kuelekea kibla ama kama hawezi basi atalala vile ambavyo ni rahisi kwake
⬆�Na mgonjwa anaposwali kwa kukaa kutokana na dharura basi swala yake ni sahihi na malipo ni kama ya yule alieswali kwa kusimama
🎙 Amesema imamu an nawawi :
📙 wamekubaliana maimamu kuwa asieweza kusimama katika swala za faradhi , aswali hali amekaa , na wala swala hatoilipa , na wala thawabu zake hazitopungua 📗
{ توضيح الاحكام : ٢/١٦٥ }
↩ Lakini pia ni wajibu kwa mgonjwa arukuu na asujudu
Lakini Ikitokezea hawezi basi ataashiria kwa kichwa chake , sehemu ya rukuu atainama kidogo na sehemu ya sijda atainama sana kidogo.
Na kama mtu atakuwa ni mgonjwa na hawezi kuashiria kwa kichwa
Atatumia macho yake kuashiria
↩ Lakini pia mgonjwa kama anaumwa sanaaa basi anaruhusika kuunganisha swala yani adhuhuri akaswali na alaasiri kabisa
Inaendelea...........
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments