Header Ads

Header ADS

VISA VYA WALIOKUA WAKITOA SADAKA

 A'ssalam alaykum Wa Rahamatullah Wa Barakatuh


🛑 *VISA VYA WALIOKUWA WAKITOA SADAKA*


======🔹🔷🔹

======


SEHEMU YA 1⃣


⭕Naam Siku ya Leo 


Nitatoa visa viwili vyenye mafunzo muhimu vinavyohusu watu waliokuwa na bustani zao zenye mazao na matunda wakawa wanatoa sadaka humo. 


⏩Hivyo Kisa kimoja kutoka katika Hadithi(Sunnah) na kimoja kutoka katika Qur-aan muda huu tutaanza na kisa kutoka katika Hadithi.


*📝Kisa kutoka katika Hadithi ni hii⤵*   


عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال  ((بيْنَما رَجُلٌ يَمشِي بِفَلاةٍ مِن الأَرض ، فَسَمِعَ صَوتاً في سَحَابَةٍ : اسقِ حَدِيقَةَ فُلانٍ ، فَتَنَحَّى ذلكَ السَّحَابُ فَأَفْرَغَ مَاءَهُ في حَرَّةٍ ، فإِذا شرجة من تِلْكَ الشِّراجِ قَدِ اسْتَوعَبَتْ ذلِكَ الماءَ كُلَّهُ فَتَتَبَّعَ الماءَ ، فإِذا رَجُلٌ قَائِمٌ في حَدِيقَتِهِ يُحَوِّلُ المَاءَ بمِسحَاتِهِ ، فقال له : يا عَبْدَ اللَّهِ ما اسْمُكَ قال : فُلانٌ، للاسْمِ الَّذِي سَمِعَ في السَّحَابَةِ ، فقال له : يَا عَبْدَ اللَّهِ لِمَ تَسْأَلُنِي عَنِ اسْمِي ؟ فَقَال : إني سَمِعْتُ صَوتاً في السَّحَابِ الذي هذَا مَاؤُهُ يقُولُ : اسقِ حَدِيقَةَ فُلانٍ لإسمِكَ ، فما تَصْنَعُ فِيها ؟ فقال : أَما إِذْ قُلْتَ هَذَا ، فَإني أَنْظُرُ إِلى ما يَخْرُجُ مِنها ، فَأَتَّصَدَّقُ بثُلُثِه ، وآكُلُ أَنا وعِيالي ثُلُثاً ، وأَردُّ فِيها ثُلثَهُ)) . رواه مسلم


 

➡Maana yake ni

Imetoka kwa Abu Hurayra (Radhiya Allahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Wakati mtu mmoja alikuwa anatembea njiani katika ardhi ya ukame ambayo haina alama ya maji, alisikia  sauti inatoka kutoka katika mawingu ikisema: "Mwagia maji bustani ya fulani". Mawingu yakaelekea upande fulani na kuanza kumwaga maji juu ya miamba tambarare. Mchiriziko ukatiririka katika mfereji mkubwa. Mtu huyo akaufuata mfereji huo hadi ukafika katika bustani na akamuona mwenye kumiliki bustani amesimama katikati yake akiyatandaza maji kwa sepeto (huku anabadilisha njia ya maji yaelekee katika sehemu nyingine ya bustani). Akamuuliza: "Ewe mja wa Allah! Jina lako nani?". Akamwambia jina lake ambalo ni lile lile alilolisikia kutoka katika mawingu. Mwenye bustani akamuuliza: "Ewe Mja wa Allah! Kwa nini umeniuliza jina langu?" Akamjibu: "Nimesikia sauti kutoka katika mawingu yaliyomwaga maji ikisema: "Mwagia maji bustani ya fulani". Nataka kujua huwa unaifanyia jambo gani?". Akasema: "Kwa vile umeniuliza nitakuambia: Hupima mapato ya bustani na kugawa thuluthi moja katika sadaka, na thuluthi moja natumia mwenyewe na familia yangu, na thuluthi moja nairudisha katika (kuizalisha) bustani")) 

↪Imepokelewa na Imaam Muslim


Itaendelea In shaa Allah


*☎+97433799776*

*RAUDHWATUL ILM*

*NDOA KATIKA UISLAM*



QURAN NA SUNNAH TZ 

WHATSAPP NO +255713849566 


TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾


websites.

http://qurannasunnahtz.blogspot.com/


Facebook page.

https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks


Instagram.

http://www.instagram.com/qurannasunnah


Whatsapp.

https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE


telegram.

https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk


YouTube

http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A




No comments

Powered by Blogger.