Header Ads

Header ADS

ZAKAH SEHEMU YA 39

 Assalam Alaykum Wa RahamatuLLAH WA Barakatuh


*KUTOA ZAKAH*


=======🔹🔷🔹

=======


_SEHEMU YA THALATHINI NA TISA_


*Kuisafirisha Zakaah*


```▶Mulamaa wengi wamekubali kuwa mali ya Zakaah (Zakaatul Maal - si Zakaatul Fitwr) inaweza kusafirishwa na kutolewa katika nchi nyingine kwa wanaoistahiki zaidi ikiwa watu wa mji anaoishi mtoaji hawaihitajii zaidi mali hiyo. Ama ikiwa katika nchi hiyo wapo wanaoihitajia, basi zipo Hadiyth zinazotujulisha kuwa Zakaah ya kila nchi wanapewa masikini wake.


Katika madhehebu ya Imaam Abu Haniyfah, wao wanasema:


"Ni Makruuh kuisafirisha mali ya Zakaah isipokuwa ikiwa kwa ajili ya kumsaidia ndugu wa nasaba mwenye kuihitajia, na hii inatokana na umuhimu wa kuunganisha undugu huo, au pia kwa ajili ya watu wenye shida sana katika watu wa nchi yake, au kwa ajili ya kuiondoa kutoka nchi ya kikafiri na kuipeleka katika nchi ya kiislam."


Madhehebu ya Imaam Ash-Shaafi’iy yanasema:


"Haijuzu kuisafirisha mali ya Zakaah na inawajibika kutolewa katika nchi iliyochumwa mali hiyo isipokuwa pakikosekana wenye kuihitajia Zakaah hiyo katika nchi hiyo".


Mu’aadh bin Jabal (Radhiya Llaahu ‘anhu) alipewa ugavana wa nchi ya Yemen na Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam), na alipotawala ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhiya Llaahu ‘anhu) alimuacha Mu’aadh aendelea kuwa gavana wa nchi hiyo. Lakini Mu’aadh (Radhiya Llaahu ‘anhu) alipompelekea ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhiya Llaahu ‘anhu) theluthi ya mali ya Zakaah, ‘Umar (Radhiya Llaahu ‘anhu) alikataa kuzipokea akamwambia:


"Sikukupeleka uwe mchotaji (wa mali) wala mpokeaji wa kodi, bali nimekupeleka kwa ajili ya kuchukua mali (ya Zakaah) kutoka kwa matajiri wao na kuzirudisha kwa masikini wao".


Mu’aadh (Radhiya Llaahu ‘anhu) akasema:


"Nisingekuletea ila kwa sababu sikumpata (masikini) anayezistahiki kuzichukua".


Itaendelea In shaa Allah```


*+97433799776*

*RAUDHWATUL ILM*


*UNGANA NASI KUPITIA TELEGRAM BONYEZA LINK IFUATAYO⤵*


 https://t.me/joinchat/AAAAAEiWeE_WKW4ORQxRzw



QURAN NA SUNNAH TZ 

WHATSAPP NO +255713849566 


TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾


websites.

http://qurannasunnahtz.blogspot.com/


Facebook page.

https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks


Instagram.

http://www.instagram.com/qurannasunnah


Whatsapp.

https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE


telegram.

https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk


YouTube

http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A



 

No comments

Powered by Blogger.