DAMU YA HEDHI
🌹🌹Assalam alaykum warahamatullah wabarakatuh
*🔷DAMU YA HEDHI.🔷*
```Ni damu nyeusi nzito yenye harufu mbaya. Inamtoka mwanamke toka sehemu maalumu katika nyakati maalumu.
Hedhi ni jambo ambalo Allaah Amewaumbia wanawake wote kama Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alivyomwambia Aaishah kama ilivyo katika sahihi mbili:
(( إن هذا أمر كتبه الله على بنات آدم....))
((Hakika hili ni jambo, Mwenyezi Mungu Amelihukumia kwa mabinti wa Aadam)).
Bali Hawwaa Amani iwe juu yake alianza kuipata. Imepokelewa kwa isnadi sahihi toka kwa Ibn 'Abbaas akisema:
“Hedhi ilianza kutoka kwa Hawwaa baada ya kushushwa toka peponi”.
Na hakuna mpaka wa uchache wala wingi wa hedhi, bali hilolinategemea maumbile ya mwanamke, kwa vile hakuna dalili yoyote sahihi toka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inayobainisha uchache wa hedhi au wingi wake.
Shaykh wa Uislamu katika Kitabu cha Al-Fataawa (21/623) anasema:
“Ama wale wanaosema kwamba wingi wa hedhi ni siku kumi na tano na uchache wake ni siku moja kama Ash-Shaafi’iy na Ahmad, au wanaosema kuwa hedhi haina mpaka maalumu kama Maaliki, hakika wao wanasema hayo, lakini halijathibiti lolote kuhusiana na hilo toka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) au Maswahaba zake. Na marejeo ya yote hayo ni maumbile ya mwanamke kamatulivyosema, na Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.”
🔷KUANZA NA KUMALIZIKA KWA HEDHI
1- Kuanza kwa hedhi kunajulikana kwa msukumo wa damu wakati wake, nayo ni damu nyeusi, nzito yenye harufu mbaya.
2- Kumalizika kwake hujulikana kwa kukatika damu, kuwepo unjano na rangi yenye kumili weusi. Na hili linatokana na mambo mawili:
(a) Ukavu; nako ni kutoka kikiwa kikavu kilichoingizwa katika njia ya uzazi. Yaani ikiwa mwanamke ataingiza kitambaa au pamba katika utupu wake, basi hutoka kikiwa kikavu.
(b) Kuwepo maji meupe yanayotoka katika njia ya uzazi wakati wa kukatika damu ya hedhi. Imepokelewa na mwachwa huru wa ‘Aaishah akisema:
“Wanawake walikuwa wakimwendea na kitambaa chenye pamba yenye unjano utokanao na damu ya hedhi, kisha wanamuuliza kamawanaweza kuswali, naye huwajibu akisema: “Msifanye haraka mpaka mwone maji meupe”.
Hapa anamaanisha kwamba wametwaharika na hedhi.```
*🔷NINI HUKUMU YA UNJANO NA RANGI YENYE KUMILI WEUSI BAADA YA KUTWAHARIKA NA HEDHI?*
```Unjano na rangi yenye kumili weusi ni maji anayoyaona mwanamke mithili ya usaha. Na hii ni baada ya kukatika damu au baada ya ukavu na kujitwaharisha. Hapo ataswali, atafunga na mumewe atamwingilia.
Dalili ya hili ni Hadiyth ya Ummu 'Atwiyyah aliposema:
“Tulikuwa - baada ya kujitwaharisha - hatushughulishwi chochote na rangi yenye kumili weusi au unjano”.```
Na Allah anajua zaidi
*NDOA KATIKA UISLAM*
*☎+97433799776*
*(Tambo)*
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments