TABIA NJEMA SEHEMU YA 11
*_رياض الصالحين (SEH:11)_* 🌹
🌺 *_TABIA NJEMA_* 🌺
▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂
🔻 _*BAADHI YA MAMBO YA KHERI*_🔻
1) kuondosha kero / udhia njiani
Sote ni wenye kutembea kutokana na pirika za kimaisha na katika safari zetu njiani tunaweza kukumbana na vitu mbali mbali ambavyo vinaweza kuwa ni kero kwa wapita njia wengine kama vile :
1) miba njiani
2) magae yachupa ambayo yanaweza sababisha kero na madhara
3) matawi au miti iliodondoka
4) njia kuchimbika na watembeaji kwa vyombo vya moto kushindwa kupita nk
👆katika Tabia njema ni kuondosha vitu njiani ambavyo vinaweza kuleta kero au kusababisha madhara kwa wengine na kuna faida nyingi ndani yake kama hadithi zifuatazo zinavyo tubainishia
➊ " Mtu mmoja alipokuwa akitembea njiani , akakuta tawi la mti lenye miba njiani , ukaliweka nyuma , Allah akamsamehe "
2) mtume ﷺ anasema " kwa hakika nilimuona mtu akitembea peponi kwa sababu ya mti alioukata kati kati ya njia , uliokuwa ukiwaudhi watu "
{ Muslim : 1914 }
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
👉 Kwaio si katika Tabia njema au Sio katika mafunzo ya kiislamu watu kuweka mawe au magogo bara barani au kuchoma matairi barabaran na kusababisha kero kwa wapitaji.
2) kuishi vyema na jirani na kupelekeana Zawadi
Sasa ivi tunaishi kila mtu na familia yake : lakini zamani wazee wetu kama itatokea mzee ameenda shamba / kijijini Amerudi na Zawadi iwe muhogo , ndizi , tungule , malimau , ndimu nk basi akifika kwake humpunguzia na jirani yake
Lakini leo hatuishi hivi : wakati uislamu unahimiza tuwe na ujirani mwema na tuwe tunapelekeana Zawadi
Mfano : umepika chakula Kizuri au chatunu { cha hamu } ambacho unahisi jirani yako anakipenda basi hakuna ubaya kumpelekea
Kwaio tunatakiwa tujengeke na Tabia hii nzuri ya kuishi kwa udugu na majirani kupelekeana zawani kwani mtume ﷺ amesema :
*_Enyi wanawake wa kiislamu , jirani asi dharau kamwe kumpa Zawadi jirani yake japo ni kwato ya mbuzi_* { bukhari : 2566, Muslim : 1030 }.
Inapofika ramadhani tuwe tunatabia yakupelekeana vyakula baina ya majirani
Inapofika skukuu pia tuwe na Tabia asubuhi yakupelekeana vyakula
👉 baba Amerudi Zanzibar kuja dar mfano Amerudi na haluwa , dagaa kavu , ubuyu basi tuwe na Tabia yakuwagaia jirani zetu
Au baba Amerudi kutoka dar kuja Zanzibar Amekuja na korosho , tungule vitunguu nk basi tujenge Tabia yakuwapunguzia majirani ili kuzidisha mapenzi baina yetu katika jamii
Au mtu umesafiri umeenda mbali umerudi umewachukulia wanao Zawadi basi mgaie japo mtoto mmoja wa jirani yako
Hili litasaidia kuzidisha mapenzi na kuondosha uhasama katika jamii.
3) Kulisha / kumnywesha mnyama
Pia katika Tabia njema ni kuwahurumia wanyama iwe kwa kuwapa chakula au kuwapa maji
Ukiona unakula na ukahisi mnyama ana njaa basi ni katika wema na yeye umpe
Au Ukiona mnyama ana kiu basi ni katika kumtendea wema umpe maji
👉 Leo hii achilia mnyama unaemkuta njiani lakini mtu ndani mwake ana mifugo iwe ngombe , paka , kuku , nk lakini hawajali kuwapa chakula wala kinywaji
Tunapaswa kuwahurumia wanyama kwani nao ni viumbe : Amesema mtume ﷺ :
*_.....kunywesha kila kilicho hai ni sadaka_* { bukhari : 2466 }.
4) kupanda miti / kuotesha matunda mbali mbali
Pia ni katika wema mtu kupanda miti an bay I watanufaika kwayo wanaadamu , wanyama , ndege nk
Kwaio kama mtu utapanda mti ambao utakuwa na faida basi kwa kila atakaenufaika kwa mti Huo ni sadaka
Amesema mtume ﷺ :
1) muislamu yoyote atakaepandikiza mti basi chochote kitakacholiwa katika mti Huo ni sadaka yake , na kitakachoibiwa ni sadaka yake ...
2) muislamu hatopandikiza mche akala mwanaadamu au mnyama au ndege isipokuwa itakuwa ni sadaka yake siku ya kiama .
3) muislamu yoyote hatopandikiza mche , wala hatolima mbegu , ikaliwa na wanaadamu au mnyama , au chochote isipokuwa itakuwa ni sadaka yake
📚 riyadhu swalihina hadithi no 135
Kwaio kama mtu atapanda mtu au matunda na watu au ndege au wanyama wakanufaika kutokana na mti huo basi hio ni sadaka.
Kama mfano umepanda mgomba au mchicha au mti wowote akapita mbuzi au ngombe au kuku au mchwa akala basi hio huwa ni sadaka na mtu anaandikiwa malipo.
_____
Itaendelea In Shaa Allah
🛑🇰🇪🇰🇪🇰🇪🇰🇪🇰🇪🇰🇪🇰🇪🇰🇪🇰🇪🛑
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments