Header Ads

Header ADS

SWALAH SEHEMU YA NNE

 

*Assalaam Alaykum Wa Rahmatul LLAAHI Wabarakaatuh*

Na'am tunaendelea na darasa letu la Swalah.

              *KUSIMAMA*
💠   *KATIKA SWALAH*   💠
          ```SEHEMU YA NNE```
==========♦========
Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiswali kwa kusimama katika Swalah zote mbili za fardhi na za Sunnah kwa kufuata maamrisho ya ALLAAH

*وَقُومُواْ لِلَّهِ قَـٰنِتِينَ*
 
*((…na simameni kwa ajili ya ALLAAH nanyi ni kuqunuti (kunyenyekea))* [Al-Baqarah, 2: 238]


Ama katika safari alikuwa akiswali Swalah za Sunnah na huku amempanda (mnyama).

Ameweka kanuni kwa ummah wake kuswali wakati wa khofu kubwa kwa kusimama juu ya mnyama. Na hili ni kwa Neno Lake ALLAAH Mtukufu:

حَـٰفِظُواْ عَلَى ٱلصَّلَوٰتِ وٱلصَّلَوٰةِ ٱلْوُسْطَىٰ وَقُومُواْ لِلَّهِ قَـٰنِتِينَ   فَإنْ خِفْتُمْ فَرِجَالاً أَوْ رُكْبَانًا فَإِذَا أَمِنتُمْ فَٱذْكُرُواْ ٱللَّهَ كَمَا عَلَّمَكُم مَّا لَمْ تَكُونُواْ تَعْلَمُونَ

*((Zilindeni Swalah, na khasa Swalah ya katikati, na simameni kwa ajili ya ALLAAH nanyi ni wenye kuqunuti (kunyenyekea)))*

((Ikiwa mnakhofu (Swalini) na hali mnakwenda kwa miguu au mmepanda. Na mtakapokuwa katika amani, basi mkumbukeni ALLAAH kama Alivyokufunzeni yale mliyokuwa hamyajui)) [Al-Baqarah, 2: 238-239]

Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) aliswali kwa kukaa wakati alipokuwa akiumwa hata akafariki. Vile vile aliswali kwa kukaa kwa mara nyingine kabla ya hivyo wakati alipojeruhiwa, na watu waliokuwa nyuma yake waliswali kwa kusimama, akawaashiria wakae nao, wakakaa (na kuswali).  Alipomaliza, akasema, Mlikuwa mnataka kufanya kama wanavyofanya wa-Fursi na Warumi wanavyofanya, wanawasimamia wafalme wao waliokuwa wanakaa. Kwa hiyo msifanye hivyo tena, kwani Imaam ni kwa ajili ya kumfuata, anapofanya rukuu fanyeni rukuu, anaposimama simameni, anaposwali kwa kukaa na nyinyi swalini kwa kukaa (nyote).

In shaa ALLAAH tutaendelea

QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566

TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾

websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/

Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks

Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah

Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE

telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk

YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A

 

No comments

Powered by Blogger.