Header Ads

Header ADS

SWALAH SEHEMU YA TATU

 A'ssalam alaykum Wa Rahamatullaah Wa Barakatuh 


Na'am tunaendelea na darasa /Somo letu la Swalah. 


               *KUSIMAMA* 

                       *NA* 

💠   *KUELEKEA QIBLAH*    💠

        ```SEHEMU YA TATU``` 

==========♦==========


         *KUELEKEA QIBLAH* 

Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuwa anasimama kuswali Swalah zote za Fardhi na za Sunnah alikuwa anaelekea upande wa Ka'abah. 

 

Naye Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) aliliamrisha hilo kwa kumwambia *"mtu aliyeswali vibaya” ((Unaposimama kuswali, fanya wudhuu sawasawa, kisha elekea Qiblah na upige Takbiyr))*[( Bukhariy, Muslim na Siraaj )] .

 

"Wakati yuko safarini, Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiswali Swalah za Sunnah na Swalah ya Witr na huku amepanda mnyama popote alipoelekea. (Mashariki au Magharibi)[ ( Bukhariy na Muslim )] 

 

 

Alikuwa akifanya hivyo ni kwasababu ya Neno Lake ALLAAH Mtukufu:

 

 فَأَيْنَمَا تُوَلُّواْ فَثَمَّ وَجْهُ ٱللَّهِ  ... 


*((Basi kokote mnakoelekea, huko kuna wajihi wa ALLAAH ))*

[Al-Baqarah: 115]

 

Kauli hii inahusiana na Hadiyth hiyo.

 

“Wakati mwengine alipokuwa anataka kuswali Swalah zisizo za fardhi juu ya ngamia wake, alikuwa akimwelekeza Qiblah, kisha akisema Takbiyr na akiswali kuelekea popote kule msafara unapoelekea.”

 

*"Alikuwa akifanya rukuu na sujuud huku amempanda mnyama kwa kuinamisha kichwa chake, na akiinamisha kichwa zaidi chini katika sujuud kuliko alivyoinamisha katika rukuu.*”[( Ahmad na Tirmithy )] 

 

*"Alipotaka kuswali Swalah za fardhi alikuwa akiteremka kutoka kwa mnyama na akielekea Qiblah*.”[( Bukhariy na Muslim)] 

 

Ama katika Swalah ya mtaharuki wa vita vilivyopamba moto, Mtume  (صلى الله عليه وآله وسلم) aliweka kwa ummah wake kanuni ya kuswali "wakiwa wamesimama na kutembea kwa miguu yao, au wakiwa wamepanda mnyama, wakielekea Qiblah audio kutokuelekea”[ ( Bukhariy na Muslim)] . Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)  akasema: *((Wanapokutana majeshi Swalah ni Takbiyr na kuashiria kwa kichwa))*[( Al-Bayhaqiy)] 

 

 

Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)  pia alikuwa akisema *((Kilichokuweko baina ya Mashariki na Magharibi ni Qiblah))* [( At-Tirmidhiy na Haakim )]

 

Jaabir (رضي الله عنه) amesema,

*"Mara moja tulikuwa na Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)  katika msafara au kikosi cha jeshi, na kulikuwa na mawingu, tukajaribu kutafuta Qiblah lakini tulikhtilafiana, kwa hiyo kila mmoja wetu akaswali kuelekea upande tofauti na kila mmoja wetu alichora mstari mbele yake ili kuweka alama mahali pake. Ilipofikia asubuhi, tukazitazama tukaona kwamba hatukuswali kuelekea Qiblah. Kwa hiyo tukamuelezea Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)  lakini hakutuamrisha tuirudie (Swalah)* na akasema:

*((Swalah yenu imetosheleza))*.[( Ad-Daara Qutniy )]

 

Mtume  (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiswali kuelekea Bayt Al-Maqdis (na Ka'abah ikiwa mbele yake) kabla ya kuteremshwa Aayah ifuatayo:

 

قَدْ نَرَىٰ تَقَلُّبَ وَجْهِكَ فِي ٱلسَّمَاء فَلَنُوَلّيَنَّكَ قِبْلَةً تَرْضَاهَا فَوَلّ وَجْهَكَ شَطْرَ ٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ وَحَيْثُ مَا كُنتُمْ فَوَلُّواْ وُجُوهَكُمْ شَطْرَهُ ...

*((Kwa yakini tukiona unavyo geuza geuza uso wako mbinguni. Basi Tutakuelekeza kwenye Qiblah ukipendacho. Basi elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtakatifu; na popote mnapokuwa zielekezeni nyuso zenu upande huo…))* [Al-Baqarah, 2: 144]

 

Ilipoteremshwa Aayah hii alielekeza uso wake Ka'abah.  Walikuwa watu katika msikiti wa Qubaa' wakiswali Swalah ya Alfajiri, alipokwenda mtu kuwaambia *"Hakika Mtume wa ALLAAH (صلى الله عليه وآله وسلم) ameteremshiwa Aayah jana usiku na ameamrishwa kuelekeza uso wake Ka'bah. Basi jueni na elekeeni huko"*. Nyuso zao zilikuwa zimeelekea Shaam kwa hiyo wakageuka (na Imaam wao akageuza uso kuelekea Qiblah pamoja nao).[( Al


 Bukhariy na Muslim )]


Tutaendelea Inshaa Allah



QURAN NA SUNNAH TZ 

WHATSAPP NO +255713849566 


TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾


websites.

http://qurannasunnahtz.blogspot.com/


Facebook page.

https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks


Instagram.

http://www.instagram.com/qurannasunnah


Whatsapp.

https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE


telegram.

https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk


YouTube

http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A



 

No comments

Powered by Blogger.