SWALAH SEHEMU YA PILI
Assalaam Alaykum Wa Rahmatul LLAAHI Wabarakaatuh.
Tunaendelea na darasa letu la Swalah tuone Swalah na Umuhimu Wake
*SWALAH*
*NA*
💠 *UMUHIMU WAKE SEHEMU YA PILI* 💠
==========♦=========
Swalah ina fadhila kubwa sana, hivyo kukosa kuswali ni kosa kubwa. Swalah ni 'amali ya kwanza itakayokaguliwa Siku ya Qiyaamah na ndio ufunguo wa Pepo. Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:-
*((’Amali ya mwanzo atakayoulizwa Muislamu Siku ya Qiyaamah kuwa kaitekeleza–na kaitekeleza vilivyo–ni Swalah. Ikiwa aliitekeleza vilivyo basi kunatarajiwa atafaulu. Ikiwa hakuitekeleza au kaitekeleza, lakini sivyo ndivyo, basi itatazamwa Swalah za Sunnah, kama alizitekeleza vilivyo. Ama ikiwa hana hata Sunnah au kaitekeleza sivyo ndivyo, basi keshapata khasara))* [Ahmad, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaaiy na Ibn Maajah].
Amesema tena (صلى الله عليه وآله وسلم):
*((Funguo za kufungulia milango ya Peponi ni Swalah))* [Muslim].
Ubaya wa kuacha Swalah ni mkubwa sana kwani ALLAAH (سبحانه وتعالى) Anasema:-
فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا الصَّلاَةَ وَاتَّبَعُوا الشَّهَوَاتِ ۖ فَسَوْفَ يَلْقَوْنَ غَيًّا
*((Lakini wakaja baada yao walio wabaya, wakaacha Swalah, na wakafuata matamanio. Basi watakuja kuta adhabu ya moto))* [19: 59].
Na kadhalika Anasema tena ALLAAH (سبحانه وتعالى) kwa kutaja habari za wasioswali pindi watakapoulizwa sababu yao ya kuwepo motoni:
مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ . قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ
*((Ni nini kilichokupelekeni motoni? Waseme: Hatukuwa miongoni waliokuwa wakiswali))* [74: 42 -43].
Na Mtume wa ALLAAH (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:-
*((Kizuizi kilichoko baina ya mtu na ukafiri ni Swalah))* [Muslim].
Kadhalika akaeleza ubaya wa mtu kutokuswali na kumfananisha na kafiri:
*((Tofauti baina yetu Waislamu na wasio Waislamu ni Swalah))* [Abu Daawuud, an-Nasaaiy na Ibn Maajah].
Baada ya kujua masuala hayo muhimu kutoka katika Kitaab na Sunnah, ndivyo vilevile tutaona umuhimu wa kuijua ‘Ibaadah hiyo vilivyo ili tuweze kuitekeleza ipasavyo. Na kwa mintarafu hiyo, tutaona kuna ulazima wa kupata mafunzo hayo kutoka katika chanzo kilichokamilika kwa dalili thaabit kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) na Maswahaba zake. Na ndio nikakichagua kitabu hiki kukitafsiri ili kumuwezesha Muislam mwenye kusoma Kiswahili anufaike na aweze kuinoa na kuiboresha Swalah yake ili aweze kufikia makusudio yaliyotajwa katika Aayah na Hadiyth mbalimbali nilizotanguliza hapo juu, na pia ili aweze kuepukana na sifa na adhabu nilizotangulia kutaja.
In shaa ALLAAH tunaendelea tena.
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.co m/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments