Header Ads

Header ADS

SWALAH UTANGULIZI

 

*Assalaam A'laykum Wa Rahmatul LLAAHI Wabarakaatuh*

🛑 *DARSA LA SWALAH*

UTANGULIZI

          *بسم الله الرحمن الرحيم*

Hakika shukurani ni Zake ALLAAH (سبحانه وتعالى), tunamshukuru Yeye, na kumtaka msaada, na tunamuomba Yeye msamaha. Tunamuomba ALLAAH (سبحانه وتعالى) Atulinde na shari za nafsi zetu na ubaya wa matendo yetu. Anayeongozwa na ALLAAH (سبحانه وتعالى) hakuna wa kumpoteza, na anayepotezwa na ALLAAH (سبحانه وتعالى) basi hakuna wa kumuongoza.

Na nashuhudia kuwa hakuna apasaye kuabudiwa ila ALLAAH (سبحانه وتعالى), Ni Mmoja tu Asiye na mshirika. Na nashuhudia kuwa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni mja Wake na ni Mjumbe Wake. Swalah na Salaam za ALLAAH zimshukie yeye, jamaa zake, Swahaba zake, na wote waliotangulia kwa wema hadi siku ya mwisho.

*Ama ba’ad,*
Namshukuru tena ALLAAH (سبحانه وتعالى) kwa kuniwezesha kuanza Darasa/Somo hili na ninaamini sana kuwa litawanufaisha Sana Wale Watakao lifuatilia na litaweza kuwasaidia kupata mafunzo sahihi ya 'Ibaadah hii adhimu ambayo itakuwa ni jambo la kwanza kabisa kwa mja kuulizwa kwalo siku ya Hesabu.

Umuhimu wa Darasa/Somo hili ni mkubwa sana, haswa kwa kuwa ni Darasa/Somo linaloelezea ‘Ibaadah hii ya Swalah kwa mapana na marefu na kwa dalili sahihi zilizothibiti kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم). Ni Darasa/Somo ambalo kwa mwenye kutaka kujua ilivyokuwa Swalah ya kipenzi chetu (صلى الله عليه وآله وسلم) kama alivyosema:- *((Swalini kama mlivyoniona nikiswali))* [Al-Bukhaariy]. Basi anapaswa kila Mtu kwenye group zetu kuwa Makini katika Kulifuatilia darasa hili.

In Shaa ALLAAH Tutaendelea tena BiidhiniLLAAHI.

QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566

TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾

websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/

Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks

Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah

Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE

telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk

YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A

 

No comments

Powered by Blogger.