Header Ads

Header ADS

TABIA NJEMA SEHEMU YA 15

 

🌹 *_رياض الصالحين (SEH:15)_*  🌹

🌺 *_TABIA NJEMA_* 🌺
▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂
📚📚
   📚

*_KUAMRISHA MEMA NA KUKATAZA MAOVU_*

uislamu unahimiza tuwe tunaamrishana mambo mema , na pindi tukiona mtu anafanya jambo baya basi tumkataze :

*_Mema_* :

→ ni kila ambalo linalotambuliwa / kuelezwa na sheria na kukubalika katika Ibada za kauli na vitendo , vyilivyodhahir na vilivyojificha

*_Maovu_*

→ ni kila ambalo limekatazwa na kuzuiwa na sheria katika aina mbali mbali za maasi kama vile kukufuru , uadui , ufisadi , uongo , udanganyifu , kusengenya na kufitinisha watu na mengineyo

💉 Kwaio Allah anatutaka tuamrishane mema na kukatazana mabaya

وَلْتَكُنْ مِنْكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ ۚ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

*_Na uwe kutokana na nyinyi umma { watu} unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa._*

Kwaio katika kuamrisha mema na kukataza mabaya basi 👇

1) tuwaite na tuwalinganie watu katika kheri

2) tuwaamrishe yale yote yalio mema

3} tuwakataze na yote ambayo ni mabaya

📚 Sharhu riyadhu swalihina { 1/525 }.

Kwaio kwanza kama unataka kumkataza mtu

Basi kwanza umlinganie katika kheri

Mfano kama mtu si muislamu basi kwanza umuite awe muislamu { Sio unaanza kumwambia atoe zaka au afunge } utamkimbiza

Baada ya hapo unatakiwa umuamrishe mtu kufanya mema na mwisho umkataze na mabaya.

Sasa katika kuamrisha na kukataza maovu kuna SHARTI zake au mambo yakuzingatia

👉 Usivamie tu ukamwambia mtu hilo haramu usifanye , au ilo halifai

Wala usivamie tu ukamwambia mtu Fanya hakuna ubaya nk

Mambo haya Tunapaswa kuyazingatia sana tena sana 👇

Katika kuamrisha mema , na kukataza mabaya kunahitajika mambo yafuatayo

1) mtu anatakiwa ajue jema na ovu { lililokatazwa }

Unapotaka kumwambia mtu Fanya jambo Fulani basi unatakiwa ujue kuwa ilo jambo ni halali na limeruhusika

Na unapomuona mtu anafanya jambo Fulani basi hupaswi kumkataza mpaka uwe na ujuzi kuwa hili analolifanya limekatazwa

👉 kama huyajui mema basi Haijuzu kuyaamrisha , kwani unaweza kuamrisha kitu uka dhani ni sahihi au jema kumbe hujui

Pia unapaswa kutambua kuwa jambo Fulani limekatazwa , kama huna ujuzi nalo basi usilikataze Kwani huenda ukakataza jambo kumbe ni jema , hivyo mtu akaacha kufanya jambo la halali kwa sababu yako

📚 Sharhu riyadhu swalihina { 1/526 }.

Kwaio unapoulizwa jambo bora useme sijui :

Kuliko kusema hapana hilo ni haramu

Au Naam , inajuzu hakuna tatizo
****

Lakini pia unapomuona MTU anafanya jambo kama wewe hulijui bora muulize mbona nimekuona unafanya jambo Fulani ??

Atakupa dalili na sababu zake : Kwaio wewe utaenda kuliulizia hilo jambo kwa wajuzi na watakupa elimu nasio kumtolea mtu ukali kuwa haramu , haifai kumbe wewe ndio hujui

*_kuuliza pia ni aina ya kujifunza_*

Kwaio kama hatujui ni bora kuuliza kuliko kuharamisha au kuhalalisha vitu au kuanza kuwakosoa watu jambo ambalo hatuna elimu nalo.

Nitakupeni mfano :

1) unaweza kwenda katika baadhi ya Misikiti ukamkuta mtu akitoka katika rukuu baada kuachia mikono , utamuona anafunga swala

Usianze tu kusema ni haramu nk : Bali muulize mbona ulivyoinuka katika rukuu umefunga mikono baada kuiachia ??? Atakupa majibu , kisha wewe nenda kauliza kwa wenye elimu ili wakufahamishe

2) unaweza Pengine kumuona mtu anaswali huku kavaa viatu

Usianze tu kusema mila za kikafiri , au anawaiga wakristo kwa kufanya ibada na viatu : Bali muulize mbona unaswali huku umevaa viatu ?? Chukua majibu yake kisha kaulizie kwa wajuzi zaidi

3) baada ya swala ukitoa salamu tu unamuona mtu anainuka anaenda zake

Usianze kuleta hadithi za ajabu kua atokae mwanzo mfuasi wa iblisi , Mara mtu kishamaliza swala hana ata mda wakumsabih mola wake , Maneno teleee : muulize kwanza kisha Pima alichokwambia

Jambo jengine ambalo unatakiwa kulizingati ni Kumnasihi mtu aswali: Unatakiwa uwe na uhakika kuwa kweli huyu mtu haswali.

Itaendelea In Shaa Allah

QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566

TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾

websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/

Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks

Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah

Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE

telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk

YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A

 

No comments

Powered by Blogger.