TABIA NJEMA SEHEMU YA 14
🌹 *_رياض الصالحين (SEH:14)_* 🌹
🌺 *_TABIA NJEMA_* 🌺
▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂
📚📚
📚
*_KUPEANA NASAHA_*
→ kawaida hakuna binaadamu ambae ni mkamilifu au ambae hakosei : Kwaio dini yetu imetutaka tuwe tunapeana nasaha pale ambao tutaona mtu anapoelekea sio kuzuri
Na huu ndio udugu wa kweli : kwani siku zote tunatakiwa tupendeleane kheri nasio kumuona mtu amezama katika maasi , au anaacha mambo ya wajibu wewe ukachekelea *_hapana_*
♻ Amesema mtume ﷺ :
*_Dini ni nasaha , tukauliza kwa nani ? Akajibu " kwa Allah , kitabu chake , mtume wake , viongozi wa waislamu na watu wote_* Muslim { 2761 }
Katika hadithi hii tunaona kuwa nasaha kwa :
① Allah
② kitabu chake
③ mtume wake
④ viongozi wa waislamu
⑤ watu wote.
1⃣
Dini ni nasaha kwa Allah , yani kuwanasihi watu katika :
① kumtakasa Allah nakufanya ibada kwa Ikhlasi
② kila siku kumkumbuka Allah kwa ulimi na moyo
a} kwa ulimi maana yake kumtaja Allah kwa wingi katika kila hali
b} kwa moyo : ni kukaa na kutafakari juu ya uumbaji wa Allah katika kuumba ardhi na mbingu , kutafakari juu ya usiku na mchana , kutafakari juu ya alama za Allah kutoka mana na jua na mwezi , nyota , majabali , miti , wanyama na vyenginevyo
③ kuilinda dini ya Allah na vitendo vya wafujaji
④ kuitangaza na kuifikisha dini ya Allah kwa waja wake kama Allah anavyosema :
وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ ۖ فَمِنْهُمْ مَنْ هَدَى اللَّهُ وَمِنْهُمْ مَنْ حَقَّتْ عَلَيْهِ الضَّلَالَةُ ۚ فَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانْظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ
*_Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Allah, na muepukeni Shetani. Basi kati yao wapo alio waongoa Allah. Na kati yao wapo ambao ulio wathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha_* An nahl { 36 }
_________
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
SWALI NA JIBU
SHEKH YUSUF MUHAMAD
_حفظه الله ورعاه._
*Tafadhali wasambazie wenzako upate ujira wa kusambaza*.
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
_________
2⃣
Dini ni nasaha kwa kitabu cha Allah Yaani :
① kuamini Habari zake na kila ambacho kimeelezwa ndani yake
② Kufahamisha maana yake na kukisomesha
→ Yaani ni nasaha juu ya kitabu cha Allah : Yaani kwa wale ambao wana ujuzi basi wawafamishe watu Quran na kuwafafanulia maana yake
Utakapo itafsiri kwa watu na kuwabainishia hukmu zake basi hii ndio nasaha juu ya kitabu cha Allah
③ Kukiweka katika sehemu iliosafi
Yani kukihifadhi sehemu iliosalama zaidi na kukiepusha kukiweka sehemu chafu chafu
④ Kuamini kuwa Quran haina mapungufu wala kasoro : haijapunguzwa wala kuzidishwa kitu
Na mtu anapaswa kuepukana na baadhi ya aqida za kishia kuwa Quran ina kasoro au mapungufu ndani yake
Yoyote Atakae sema kuwa Qurani inamapungufu au kasoro basi ameikadhibisha kauli ya Allah aliposema :
إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ
*_Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda._* {15:9}
________
Hapo katika kueka msahafu chini Jamani hakuna ubaya wowote wala hakuna zambi
Hata kama mfano umeweka katika ardhi madamu io sehemu ni safi na haina uchafu wowote.
3⃣
Kwa mtume wake : inajumuisha mambo mawili
(❶) kuamini ujumbe wake wote , na kuwa Allah amemtuma kwa viumbe wote kama anavyosema Allah :
وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِلْعَالَمِينَ
*_Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote._* {21:107}
→ na katika kadhia hio yanaingia mambo yafuatayo :
① kuamini kila ambacho mtume wa Allah ametueleza na kutufundisha
② tunatakiwa tumfuate kwa kila ambacho ametuelekeza : unatakiwa umfanye mtume ndio Imamu na kigezo chako katika kila Ibada
③ kupambana na watu wa bidaaa kama wao wanavyopambana na sunna
④ kuwakirimu maswahaba zake , kuwatukuza na kuwa penda
→ Tunapaswa kunasihiana juu ya kuwatukuza maswahaba wa mtume na kujiepusha na wale wote ambao wanaowatukana na kuwadhoofisha au kuwafanya maswahaba ni kama watu wa kawaida.
Allah anajua zaidi
No comments