TABIA NJEMA SEHEMU YA 13
🌹 *_رياض الصالحين (SEH:13)_* 🌹
🌺 *_TABIA NJEMA_* 🌺
▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂
🔻 *_KUDUMU KATIKA IBADA_*
→ Uislamu unatuhimiza tudumu katika vitendo vyema , tumesoma kuwa tunatakiwa tufanye mambo ya kheri lakini pia tukajifunza kuwa tunatakiwa tufanye ibada kwa kadri ya uwezo wetu bila kuzikalifisha nafsi zetu
Pia dini yetu inatutaka tufanye ibada / matendo mema ambayo ni endelevu :
a} kama unaswali usiku basi uwe unadumu na ibada hio
b} kama kila siku unasoma Quran au kuleta adhkari basi iwe ndio mwenendo wako
c} kama unapenda kufunga jumaatatu na Alhamis au masiku meupe basi usikatishe njiani
→ Tunatakiwa tunapoamua kufanya Ibada Fulani basi iwe ni endelevu kwani Amali bora inayopendeza kwa Allah ni ile yenye kudumu hata kama ni ndogo na ndipo Allah aliposema :
*_Na muabudu mola wako mpaka ikufikie hio yakini { mauti }_* [15 : 99]
💉 Kwaio tunatakiwa tushikamane na vitendo vyema mpaka umauti utufikie nasio leo tunaswali kesho tunaacha , leo tunafanya jema hili Halafu tunaliacha : Tunapaswa tushikamane na Ibada mpaka mtu ahadi yake yakurudi kwa mola wake ifike na ndipo mtume ﷺ alipotoa usia nakusema :
" Ewe Abdullah usiwe kama Fulani , alikuwa akiswali { Akisimama } usiku , na akaacha kuswali usiku " bukhari { 1156 }
Itaendelea In Shaa Allah
•┈┈•┈┈•⊰✿📚✿⊱•┈┈•┈
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments