Header Ads

Header ADS

FUNGA YA ASHURA SEHEMU YA 3

Assalam Alaykum Wa RahamatuLLAH wa Barakatuh



*🌹FUNGA YA ASHURA🌹*


*3-Sababu Ya Kufunga Siku Ya 'Aashuraa*  

عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ قَدِمَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْمَدِينَةَ فَرَأَى الْيَهُودَ تَصُومُ يَوْمَ عَاشُورَاءَ فَقَالَ: ((مَا هَذَا ؟)) قَالُوا : هَذَا يَوْمٌ صَالِحٌ، هَذَا يَوْمٌ نَجَّى اللَّهُ بَنِي إِسْرَائِيلَ مِنْ عَدُوِّهِمْ فَصَامَهُ مُوسَى، قَالَ: ((فَأَنَا أَحَقُّ بِمُوسَى مِنْكُمْ)) فَصَامَهُ وَأَمَرَ بِصِيَامِهِ

Imepokelewa na Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alielekea Madiynah akawaona Mayahudi wanafunga swawm siku ya 'Aashuraa, akasema: ((Nini hii?)) (yaani kwa nini mnafunga?) Wakasema: Hii ni siku njema, hii ni siku Allaah Aliyowaokoa wana wa Israaiyl kutokana na adui wao, na Muwsaa alifunga swawm siku hii. Akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Mimi nina haki zaidi juu ya Muwsaa kuliko nyinyi)). Akafunga swawm siku hiyo na akaamrisha ifungwe" [Al-Bukhaariy]    


Lakini Nabiy wetu (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuamrisha tukhitilafiane na Mayahudi kwa kufunga swawm siku moja kabla yake.

روى عَبْدَ اللَّهِ بْنَ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قال : "حِينَ صَامَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَوْمَ عَاشُورَاءَ وَأَمَرَ بِصِيَامِهِ قَالُوا يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّهُ يَوْمٌ تُعَظِّمُهُ الْيَهُودُ وَالنَّصَارَى فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((فَإِذَا كَانَ الْعَامُ الْمُقْبِلُ إِنْ شَاءَ اللَّهُ صُمْنَا الْيَوْمَ التَّاسِعَ)) قَالَ فَلَمْ يَأْتِ الْعَامُ الْمُقْبِلُ حَتَّى تُوُفِّيَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ". رواه مسلم 


*Imepokelewa na Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Alipofunga swawm Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) siku ya 'Aashuraa na akaamrisha ifungwe wakasema: Ee Rasuli wa Allaah! Hii ni siku wanayoitukuza Mayahudi na Manaswara. Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Ikifika mwakani In shaa Allaah tutafunga swawm siku ya tisa pia)). Akasema (Ibn 'Abbaas) haukufika mwaka uliofuata ila alifariki Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) [Muslim]* 


Kwa hiyo ni bora kufunga swawm siku ya tisa na kumi (9, 10 Al-Muharram) na kama mtu hakujaaliwa basi afunge swawm siku ya kumi na kumi na moja (10, 11 Al-Muharram), na kama hakujaaliwa basi asikose kufunga siku ya kumi pekee (10 Al-Muharram) ili asikose fadhila zake kabisa.

 

Itaendelea sehemu ya mwisho,maudhui:

4-Bid'ah Katika Siku Ya 'Aashuraa


*+97433799776*

*RAUDHWATUL ILM*



QURAN NA SUNNAH TZ 

WHATSAPP NO +255713849566 


TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾


websites.

http://qurannasunnahtz.blogspot.com/


Facebook page.

https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks


Instagram.

http://www.instagram.com/qurannasunnah


Whatsapp.

https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE


telegram.

https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk


YouTube

http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A



 

No comments

Powered by Blogger.