SWALAH SEHEMU YA TANO
*Assalaam Alaykum Wa Rahmatul LLAAHI Wabarakaatuh*
tunaendelea na darasa letu la Swalah na Leo tutagusia *Niyyah, Takbir ya kuhirimia Swalah na tutagusia Swalah kulielekea Kabur*
*SWALAH*
💠 *NIYYAH KATIKA SWALAH* 💠
```SEHEMU YA TANO```
===========♦==========
*Niyyah* ni Kukusudia/Kusudio, kwa hiyo mtu anayetaka kuswali, hutia niyyah akilini tayari kwa ajili ya hiyo Swalah pamoja na yanayohusika nayo ya sifa zake, mfano kama ni Swalah ya kipindi kipi, je, ni Swalah ya faradhi au Sunnah. ndipo huleta hivi vyote katika niyyah yake pamoja na Takbiyr ya mwanzo".
Na alikuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema:-
*((Vitendo vinategemea (vinalipwa kwa) nia na kila mtu atapata kwa mujibu wa kile alichokusudia))*.[( Muslim, Abu Dawuud na Ibn Khuzaymah )]
⏯ Hadiyth inaashiria kwamba hakuwa akianza (Swalah) kwa maneno ya baadhi ya watu: *"Nawaytu Uswalliy… n.k"* ambayo imekubalika kuwa ni bid'ah (uzushi). Bali wamekhitilafiana kama ni bid'ah njema au mbaya ambayo tunasema: Hakika bid'ah zote katika ibada ni upotofu, kutokana na kauli ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) *((…na kila bid'ah ni upotofu na kila upotofu ni motoni))*. Lakini hapa sipo mahali pa maelezo marefu ya mas-ala haya.
Hivyo basi jua kuwa niyyah mahala pake ni Moyoni na sio Kuitamka kama vile tulivyozoea Wengi Wetu.
💠 *TAKBIYR* 💠
=======================
Kisha Yeye Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akianza Swalah kwa kusema:-
*‘ALLAAHU Akbar’*
Alimuamrisha 'mtu aliyeswali vibaya' afanye kama ilivyotajwa na akamwambia: *((Hakika Swalah ya mtu haikamiliki hadi awe ametawadha kwa wudhuu uliyokamilisha viungo vya mwili kisha akasema ALLAAHU Akbar))*.[ ( At-twabaraaniy ikawa na Isnad Sahih )]
Pia alikuwa akisema:
*((Ufunguo wa Swalah ni Twahara, inaharamishwa (inaanzwa) na Takbiyr na inahalalishwa (inamalizikia) na Tasliym))*.[( Abu Dawuud, At-Timidhiy na Al-Haakim )]
✳ *Maelezo*
Maana hasa ya *'inaharamishwa na Takbiyr'*, ni vitendo vyote ambayo ALLAAH Ameviharamisha wakati huo Wa Swalah. na *"inahalalishwa na Tasliym''* ina Maana ni yale yote yaliyoruhusiwa nje ya Swalah. Kama vile Hadiyth ilivyothibitsha kuwa mlango wa Swalah umefungwa, hakuna mwenye kuabudu anaweza kufungua isipokuwa kwa Twahara, imethibitisha pia kuwa Swalah haiwezi kufunguliwa (kuanzishwa) isipokuwa kwa Takbiyr na haiwezi kumalizika bila ya Tasliym. Hii ni rai iliyokubalika kwa wengi wa Maulamaa.
Pia Mtume صل الله عليه وسلم *"alikuwa akipandisha sauti yake kutamka Takbiyr hadi walio nyuma yake walimsikia*"[( Ahmad na Al-Haakim )].
Lakini *"anapokuwa Mtume (صل الله عليه وسلم) ni Mgonjwa Abu Bakr alikuwa akipandisha sauti yake kutamka Takbiyr kwa niaba ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)*.[( Muslim na An-Nasaaiy )]
Alikuwa akisema pia:
*((Imamu anaposema: ALLAAHU Akbar, basi sema: ALLAAHU Akbar))*.[( Ahmad na Al- bayhaqiy )]
💠 *KUNYANYUA MIKONO* 💠
========================
Alikuwa Mtume (صلى الله عليه وسلم) mara nyingine akinyanyua mikono pamoja na *Takbiyr*. Mara nyingine baada ya *Takbiyr* na mara nyingine kabla yake.[( Bukhariy na An-Nasaaiy )]
Alikuwa akiinyanyua kwa kuvinyosha vidole vyake (sio kwa kuvitawanya wala kuvibana pamoja) na "alikuwa akiiweka (mikono) sambamba na mabega yake" ingawa kwa nadra, *"alikuwa akiinyanyua hadi ifikie sawa na (ncha ya juu ya) masikio yake*".[( al-Bukhariy na Abu Dawuud)
*KUWEKA (KUFUNGA) MKONO*
*WA*
*KULIA JUU YA MKONO*
*WA*
*KUSHOTO*
*NA*
💠 *KUAMRISHWA KWAKE* 💠
============♦============
"Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wa kushoto na alikuwa akisema:
*((Sisi, Mitume, tumeamrishwa kukimbilia kufungulia Swawm, kuchelewa (kula) daku na kuweka mkono Wa kulia juu ya mkono Wa Kushoto katika SWALAH))*.[Ibn Hibban) ]
Vile vile: *alimpitia mtu aliekua akiswali alieweka mkono wake Wa Kushoto juu ya mkono Wa kulia, akamvuta kuondosha Kisha akauweka Wa kulia juu ya Kushoto"* [ Ahmad na Abu Dawuud ]
*SWALAH*
💠 *KUELEKEA KABURI* 💠
=========♦==========
Mtume alikuwa akikataza kuswali kwa kuyaelekea makaburi akisema-:
*((Msiswali kuelekea makaburi na msiyakalie ))* [(Muslim, Abu Dawuud na Ibni khuzaymah ]
Tutaendelea In shaa Allah
*☎+97433799776*
*RAUDHWATUL ILM*
📗〽〽〽〽〽〽〽〽〽📗
QURAN NA SUNNAH TZ
WHATSAPP NO +255713849566
TEMBELEA KWENYE MITANDAO KWA MASOMO MENGINE ZAIDI👇🏾
websites.
http://qurannasunnahtz.blogspot.com/
Facebook page.
https://m.facebook.com/Quran-na-sunnah-tz-100238655597178/?ref=bookmarks
Instagram.
http://www.instagram.com/qurannasunnah
Whatsapp.
https://chat.whatsapp.com/FfEoBrL4bmr0vbNQhNPKFE
telegram.
https://t.me/joinchat/3WW1yKOS9-MzN2Zk
YouTube
http://m.youtube.com/channel/UC1i0tOe8KZP7L0-rOisIb2A
No comments